Jos Van Lange akitoa mada wakati wa mkutano wa
wajasiliamali ulioandaliwa na benki ya NMB. Zaidi ya wafanyabiashara 300
wa Mkoa wa Mtwara walihudhuria mkutano huo ambapo pia walipewa mafunzo
ya jinsi ya kukuza biashara zao
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imeendesha mafunzo kwa wajasiliamali zaidi ya 6200 wa Wilaya na Mikoa yote nchini yenye lengo la kuwapa ujuzi wa jinsi ya kukuza biashara zao kwa maendeleo ya kiuchumi nchini.
Wafanyabiashara hao wamekua wakipewa mafunzo yanayohusu bidhaa zinazotolewa na NMB kama jinsi ya kutunza vitabu vya mahesabu, elimu ya masoko na pia elimu ya mlipa kodi na matumizi bora ya mikopo wanayopatiwa na benki ya NMB.
Akizungumza kwenye moja ya mikutano ya wafanyabiashara Mkoani Mtwara ambapo zaidi ya wajasiliamali 300 walihudhuria. Kaimu Mkuu wa kitengo cha biashara za wateja NMB Donatus Richard -alisema kuwa katika kuwajali Wateja wake wadogo na wakati, NMB imekuwa ikiendesha mafunzo ya wajasiliamali nchi nzima ili kuwapa elimu ya jinsi ya kukuza biashara zao.
“kuna wafanyabiashara ambao walianza na mitaji midogo sana, wameanza kwa kukopa shilingi laki 5 tu na kuziwekeza kwenye biashara, kupitia mafunzo haya na pia ushauri tunaowapa, wamekuza mitaji yao na wengine sasa wanakopa mabilioni ya Fedha kutoka NMB.” Alisema Donatus.
Mafunzo hayo ya wajasiliamali yalifanyika kwa klabu za biashara za katika kila Mkoa na Wilaya ambapo Viongozi mbali mbali wa kiserikari na viongozi wa wafanyabiashara wamekua wakihudhuria hafla hizi. Zaidi ya wafanyabiashara 6200 wamepata na kunufaika na mafunzo kutoka NMB.
NMB imefanya mikutano ya business club 31 nchi nzima zenye wanachama zaidi ya 200 ambao wamekuwa wakifaidika na mafunzo mbalimbali kutoka NMB yanayohusu bidhaa zinazotolewa kwao na benki kama jinsi ya kutunza vitabu vya mahesabu, elimu ya masoko na pia elimu ya mlipa kodi.
Lakini pia Zaidi ya wajasiliamali 1000 walipata nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa mikutano hii kwa wajasiliamali wenzao.
Bwana Donatus alisisitiza kwamba lengo kuu la vilabu hivi vya biashara vimeundwa kuhakikisha wafanyabiashara nchini wanakuza mitaji yao, kuajiri watanzania wengi zaidi na pia kuchangia uchumi wa taifa hili kupitia ulipaji kodi.
No comments:
Post a Comment