Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa nasaha kwa wazee wa Mkoa wa Rukwa na waandishi wa habari (hawapo pichani). (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa).
Na Mwandishi wetu, Rukwa
Ameonya kuwa kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wazito kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari jambo linalopelekea wadau wa maendeleo walio nje ya Mkoa kutofahamu fursa zilizomo katika mkoa na changamoto zinazopatikana ili watoe ushirikiano katika kuzitatua changamoto hizo.
“Kwa Mkoa huu wa Rukwa waandishi wa habari Ruksa kufanya kazi yenu vizuri, Vyombo vya habari ni fursa, wao ndio watakaoiambia dunia kuwa Rukwa iko hivi, hakuna mwandishi atakayewekwa ndani katika mkoa huu, wao ni wadau muhimu sana katika maendeleo na sio watu wa kuwaweka pembeni katika kufikisha ujumbe kwa jamii,” alisisitiza
Ameyatamka hayo wakati wa kikao chake na wazee wa Mkoa wa Rukwa pamoja na baadhi ya viongozi wa dini kilichowaalika waandishi wa habari ili kuijua mipango na mikakati yake katika kuonafursa za Rukwa zinatangazwa kitaifa na kimataifa.
Lakini pia hakusita kuwatahadharisha waandishi hao kuwa anayekwenda kinyume na miiko ya uandishi na kugeuza misingi ya kazi yake, hatokuwa na nafasi ya kufanya kazi katika Mkoa na kuongeza kuwa mwandishi wa habari hapaswi kuwa wakala wa vyama vya kisisasa na kuacha kuandika mazuri yanayotendwa na serikali ya awamu ya tano.
No comments:
Post a Comment