HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 05, 2017

WAZAZI MBURAHATI SACCOS YAIVA, KUPATA HATI YA USAJILI HIVI KARIBUNI

Mwenyekiti wa muda wa Wazazi Mburahati Saccos, John Mapunda akifungua mkutano wa wanachama wa Saccos hiyo, uliofanyika kwenye ukumi wa Jengo la Kitegauchumi la CCM, Mburahati, Dar es Salaam, jana. Amesema ameamua yeye na wenzake kuanzisha ushirika huo wa Akiba na mikopo siyo kwa maslahi ya kisiasa bali kuwasaidia kuwasaidia kiuchumi wanachama wa Jumuiya ya Wazazi katika Kata ya Mburahati ili nao waweze kuwa na maisha bora wakiwa ni miongoni mwa Watanzanaia wenye mahitaji hayo. Kushoto ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo ambaye alifika kwenye mkutano huo kutoa mafunzo ya namna bora ya kuanzisha na kuendesha Saccos. Kulia ni Mhazini wa muda Boniface Chigenda na Katibu wa muda Sofia Kiroboto.
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo akitoa mafunzo ya namna bora ya kuanzisha Saccos na kuifanya idumu wakati wa mkutano huo. Amesema Saccos hiyo kwa sasa imeshatimiza masharti yote ya kupatiwa usajili na inapatiwa usajili huo hivi karibuni, alisema katika Kadirio lake Saccos hiyo inatarajia kupata zaidi ya Sh. milioni 13 kutokana na ada na michango ya wanachama ambao hadi sasa wamefikia 68, pia kufanya matumizi ya zaidi ya Sh. milioni 13 na kubaki na ziada ya zaidi ya Sh. milioni 29.
Kitabu au Masharti ya Saccos hiyo. 
Baadhi ya wanachama wa Saccos hiyo wakisikiliza Ofisa huyo kwa makini.
Mwanachama wa Saccos hiyo Dismas Shirima akiuliza swali.
Mwanachama wa Saccos hiyo Mtindi Mbega akiuliza swali
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo (kushoto), akimsikiliza kwa makini Mwanachama wa Saccos hiyo Justin Kaijage wakati akiluzwa swali
Mwenyekiti wa muda wa Saccos hiyo John Mapunda na Katibu wake Sofia Kiroboto wakifuatilia kwa karibu wakati wanachama wakiuliza maswali
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo akijibu maswali.
Wanachama wakichangamkia kulipa ada.
Mtoto wa mmoja wa wanachama wa SACCOS akijiburudisha kwa soka wakati mkutano ukiendelea.
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo (kulia) akiagana na wanachama waanzilishi wa Saccos hiyo, Dickson Tungaraza, baada ya kikao kumalizika. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

No comments:

Post a Comment

Pages