HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 18, 2017

IGP SIRRO APOKEA MSAADA VIFAA TIBA

 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza mmoja kati ya madaktali wa hospitali ya Jeshi hilo iliyopo barabara ya Kilwa, wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vilivyotolewa na serikali ya Marekani, vifaa vyenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni mbili, kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaofika  hospitalini hapo kwa ajili ya  matibabu.
 Mkuu wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi (SACP) Paul Kasabago (kushoto), akitoa neno la shukurani wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vilivyotolewa na serikali ya Marekani, kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaofika katika  hospitalini ya Jeshi hilo iliyopo barabara ya kilwa kwa ajili ya matibabu. 
Baadhi ya vifaa tiba vilivyotolewa na serikali ya Marekani na kukabidhiwa Jeshi la Polisi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaofika katika  hospitalini ya Jeshi hilo iliyopo barabara ya kilwa kwa ajili ya matibabu. Picha na Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

Pages