Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiwatahadharisha wanafunzi
juu ya kosa la kupata mimba wakiwa shuleni wakati alipotembelea shule
hiyo ya Sekondari Kirando Wilayani Nkasi.
Nkasi, Rukwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakuu
wa wilaya na wakuu wa shule Mkoani humo kumkamata na kuwaweka ndani wazazi na mwanafunzi
yeyote wa kike atakayebainika kuwa na mimba hadi hapo watakapomtaja
aliyesababisha mimba hiyo.
Amesema kuwa kumekuwa na tabia ya kumalizana kienyeji huko
majumbani na matokea yake watuhumiwa hawafikishwi sehemu husika ili waweze
uwajibishwa na hatimae kupunguza kasi hiyo ya mimba kwa wananfunzi.
“Mwalimu Mkuu unapogundua tu kwamba mwananfunzi ana mimba
mweke pembeni ita wazazi wake, washirikishe polisi wawachukue wawekwe ndani kwa
muda wa masaa 48, hadi hapo watakapomtaja muhusika wa mimba hiyo, ukifanya
hivyo mara kadhaa mabadiliko yatatokea,” Amesisitiza
Ametoa agizo hilo baada ya kusomewa taarifa ya shule ya
sekondari Kirando, Wilayani Nkasi wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa
maabara wa shule hiyo pamoja na na kuongea na wanafunzi, taarifa iliyobainisha
kupatikana kwa mimba saba kwa kipindi cha Januari hadi oktoba mwaka huu na kesi
zote zipo polisi.
Halikadhalika alitahadharisha kuwa shule yeyote
atakayoitembelea katika ziara yake hiyo ya kujitambulisha katika Halmashauri
nne za mkoa huo, ihakikishe inabainisha hatua zilizochukuliwa kwa watuhumiwa na
zilipofikia na si kueleza tu idadi ya kesi na kuwepo kwa kesi hizo polisi.
Kwa upande wake mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kirando Erneo Mgina amesema kuwa kati ya wanafunzi saba
waliopata ujauzito wanafunzi watatu ni wa “A – Level” na wanne ni wa “O – Level”
na kueleza kuwa wengi wao hupata mimba wakati wa likizo na huwabaini pale tu
wanaporudi shule na kuwapima.
IMETOLEWA NA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA
No comments:
Post a Comment