Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)
akipokea zawadi aliyopewa na Chuo Kikuu cha Guangdong kilichopo Jijini Guangzhou China, wakati wa
ziara ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China, zawadi
hiyo ilikabidhiwa na kiongozi wa Msafara , Mheshimiwa. Augustino Masele
(kushoto) na wengine ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki
mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji wao wa kazi nchini China katika tukio
lililofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza
na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki mafunzo ya
kuwajengea uwezo wa utendaji wao wa kazi nchini China katika kikao
kilichofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea
zawadi kutoka kwa Kiongozi wa Msafara, Mheshimiwa Augustino Masele (kushoto)
iliyotoka Chuo Kikuu cha Guangdong kilichopo
Jijini Guangzhou China, wakati wa ziara ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania nchini China, katika tukio lililofanyika leo ukumbi wa
Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa tatu
kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji wao
wa kazi nchini China katika tukio lililofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini
Dodoma.
No comments:
Post a Comment