Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi Meja Jenerali Issa
Suleiman Nassoro wa Misri (katikati) na Balozi Abdulrahman Kaniki wa
Zambia Ofisini kwake mjini Dodoma Novemba 16, 2017. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa
Tanzania nchini Misri, Balozi Meja Jenerali Issa Suleiman Nassoro na
Balozi Abdulrahman Kaniki wa Zambia, ambapo amewataka wakaimarishe
mahusiano baina ya nchi zote mbili.
Amekutana
na Mabalozi hao Balozi leo (Alhamisi, Novemba 16, 2017) katika Ofisi ya
Waziri Mkuu iliyopo Barabara ya Reli na Mahakama mijini Dodoma na
kuwasisitiza wakaboreshe shughuli za Kidiplomasia kati ya Tanzania na
nchi za Misri na Zambia.
Pia
Waziri Mkuu amewataka Mabalozi hao wakahakikishe wanatangaza vivutio
vya utalii vilivyopo nchini, ukiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za
wanyama, fukwe pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo nchini hususan
katika sekta ya viwanda.
Amesema
licha ya kutangaza fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii pamoja na
kuboresha biashara baina ya Tanzania na nchi za Misri na Zambia pia
wakawashawishi wawekezaji waje wawekeze katika sekta mbalimbali nchini
ikiwemo ya viwanda.
Waziri
Mkuu amesema Tanzania ni nchi salama yenye amani na utulivu wa kisiasa,
pia Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji jambo ambalo
litawawezesha wawekezaji watakaokuja kuwekeza nchini kupata tija.
Pia Waziri Mkuu amewataka Mabalozi hao wahakikishe wanakwenda kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amewataka Mabalozi hao kwenda kukutana na kufanya
mazungumzo na Watanzania waishio kwenye nchi hizo na kuwasisitiza waishi
kwa kuzingatia sheria za nchi husika. Pia wawaunganishe pamoja na
kuwashauri waje kuwekeza nchini.
Kwa
upande wao Mabalozi hao wamesema watahakikisha wanayafanyia kazi
maelekezo yote waliyopewa na Waziri Mkuu ikiwa ni pamoja na kwenda
kutafuta wawekezaji ili wawe kuwekeza katika sekta ya viwanda na
kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hizo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, NOVEMBA 16, 2017.
No comments:
Post a Comment