HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 07, 2017

NAIBU WAZIRI NDITIYE AFANYA ZIARA JNIA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akipata maelezo kutoka kwa Depot Meneja wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy, Mohamed Ngayahika wakati alipofanya ziara katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam Desemba 7, 2017. (PIcha na Francis Dande).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Richard Mayongela, akitoa ufafanuzi wakati Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, alipofanya ziara katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akitoa maelekezo alipotembelea Depot ya Kampuni ya Mafuta ya Puma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akiongozana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela, wakati wa ziara yake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Naibu Waziri akisaini kitabu cha wageni alipofika katika Depot ya Puma Energy.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzanian Air Services, Joannis Samaras (kulia), akitoa historia fupi ya kampuni hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye.
Fundi Mwandamizi wa Kampuni ya Tanzanian Air Services, Mohamed Mashika, akitengeneza ndege ndogo.
Fundi Mwandamizi wa Kampuni ya Tanzanian Air Services, Mohamed Mashika, akiwa kazini.
Naibu Waziri akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Tanzanian Air Services.
Naibu Waziri akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Tanzanian Air Services,
Naibu Waziri akiwa akitembelea eneo la Kampuni ya kutoa huduma za usafiri wa anga ya Tanzanian Air Services.
Ziara.
Naibu Waziri akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), baada ya kumaliza kwa ziara yake ambapo pamoja na mambo mengine alitoa maagizo ya kuanza kwa mchakato wa kuzifutia hati miliki Depot ya Kampuni ya Mafuta ya Puma pamoja na Kampuni ya Tanzanian Air. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela

No comments:

Post a Comment

Pages