WAZIRI MKUU Kassima
Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika
uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.
Aliyasema hayo jana (Jumatatu
Januari 29, 2018) alipozungumza baada ya mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi
za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Katika Mkutano huo
ambao Waziri Mkuu alimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, alisema nchi za
Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na vijijini.
Waziri Mkuu alisema
nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo la kuinua kiwango cha
maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.
Alisema nchi za
Afrika zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia ya Afrika
Mashariki (EAC) na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia amapendekezo ya
kuimarisha uzalishaji wa umeme.
“Tanzania iko vizuri
kwa sababu ina vyanzo vingi vya kuzalisha umene na sasa inamikakati ya
kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na kukaribisha wawekezaji
kwenye maeneo mbalimbali.”
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema
maelengo ya mkutamo huo yalikuwa ni kupokea taarifa za tume mbalimbali
zilizoundwa katika kikao kilichopita.
Alisema miongoni mwa
taarifa hizo ni pamoja na ya tume iliyokuwa
inashughulikia masuala ya usalama na amani katika Bara la Afrika.
“Tume nyingine
ilihusika na mapitio ya namna kuhamasisha nchi za Afrika kufikia kwenye
maendeleo na nyingine ilikuwa inahamasisha mahusiano ya nchi kupitia kwenye
Jumuia zilizopo ndani ya Bara la Afrika kama SADC.”
Pia Waziri Mkuu
alisema mkutano huo ulifanya mapitio ya mapendekezo ya namna nchi za Afrika
zinavyoweza kupata mitaji kupitia michango ya nchi mbalimbali, ambapo kanuni ziliandaliwa ili kuwezesha kila nchi
kuchangia katika mfuko mkuu wa Umoja wa Afrika.
Alisema Tanzania ilihusika kutoa mchango juu suala la amani na
usalama katika nchi za Afrika. ambapo kila nchi inawajibika kujilinda yenyewe
na kulinda nchi jirani pamoja na Jumuia zake.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU
JUMANNE,
JANUARI 30, 2018.
No comments:
Post a Comment