Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia),
akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Mpira wa Miguu yajulikanayo
kama Masauni-Jazeera Cup, Juma Suabu (wapili kushoto), msaada wa taa za
uwanjani zitakazotumika wakati wa mashindano hayo yanayofanyika nyakati za
usiku katika kila mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika jimbo hilo. Wengine ni
Diwani wa Wadi ya Kikwajuni, Ibrahim Ngassa (wakwanza kushoto), Mwakilishi wa
Jimbo la Kikwajuni, Saleh Nassoro Jazeera (watatu kulia) na Diwani wa Wadi ya
Raha Leo, Mbarouk Hanga. Picha na Mpiga Picha Wetu).
Mwananchi wa Jimbo la Kikwajuni
Mtaa wa Mji Mpya, Mzee Issa (kulia), akimshukuru
Mbunge wa jimbo hilo ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, baada ya kutoa msaada wa bomba zitakazotumika kupeleka
maji kwa wakazi wa jimbo hilo ikiwa lengo ni kukamilisha ahadi alizoahidi
Mbunge huyo wakati wa kampeni.Picha na Mpiga Picha Wetu
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni
ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (watatu kulia), na Mwakilishi wa
jimbo, Saleh Nassoro Jazeera wakimkabidhi Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama
cha Mapinduzi (UVCCM) Yusuf Mwindadi, kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya
shughuli za jumuiya hiyo.
Mwakilishi wa Jimbo la
Kikwajuni, Saleh Nassor Jazeera, akimkabidhi msaada wa komputa kiongozi wa
vijana jimboni Kikwajuni, Abdul Simai, kwa ajili ya shughuli mbalimbali
zinazohusu vijana wa jimbo hilo.Wengine meza kuu ni viongozi wa jimbo hilo
wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la
Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (wanne kulia).
Mwakilishi wa Jimbo la
Kikwajuni, Saleh Nassor Jazeera, akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Kundemba kiasi cha shilingi
Laki Tano (500,000) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ununuzi wa vifaa katika kujiandaa na mashindano.Wengine meza
kuu ni viongozi wa jimbo hilo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia).
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni
ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni, akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa Hadhara ambapo lengo la
mkutano huo ni kuelezea ahadi zilizotekelezwa na mipango ya kuliletea maendeleo
jimbo hilo.Wengine meza kuu ni viongozi wa jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment