HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 05, 2018

LUSHOTO WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUSAIDIA SEKTA YA AFYA




Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani Lushoto ambapo pamoja na kusikiliza kero zao aliishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuijali kata hiyo kwa kupeleka fedha milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kisasa katika Kata ya Mlola ambapo kati ya hizo milioni 300 kwa ajili ya kununulia vifaa wakati kituo hicho kitakapomalika huku milioni 400 zikiwa tayari wameingiziwa tayari kwa ajili ya ujenzi huo.

Diwani wa Kata ya Mlola (CCM) akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi.
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia aliyekaa kulia akiandika baadhi ya kero alizoelezwa na wananchi hao ili kuweza kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Mkazi wa Kijiji hicho Kata ya Mlola wilayani Lushoto akimuuliza swali Mbunge huyo.
Mkazi wa Kijiji hicho akimuuliza swali Mbunge wa Jimbo hilo
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katikati akiagana na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Mlola wilayani Lushoto,Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi,Elmerick Joseph mara baada ya kumalia mkutano wa hadhara katikati ni diwani wa kata hiyo
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akisalimiana na wakina mama wa Kijiji hicho mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara.

Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katikati akiwasilikiliza wananchi wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara.

No comments:

Post a Comment

Pages