HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 26, 2018

TIDO MHANDO AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mkurugenzi wa zamani wa TBC, Tido Mhando, akisindikizwa na polisi kuingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam alipofikishwa kwa mashtaka ya matumizi mabaya ya Madaraka na kuachiwa kwa dhamana. (Picha na Habari Mseto Blog).
 Mkurugenzi wa zamani wa TBC, Tido Mhando, akisindikizwa na polisi kuingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa zamani wa TBC, Tido Mhando akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Tido Mhando amefikishwa mahakamani leo jijini Dar es Salaam kwa mashtaka ya matumizi mabaya ya Madaraka.

Tido Mhando, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media alifikishwa katika mahakama ya Kisutu mapema leo Ijumaa, na kusomewa dhidi ya matumizi mabaya ya ofisi.

Anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, wakati alipokuwa akilitumikia shirika hilo la Utangazaji la Serikali TBC, pamoja na kulitia hasara ya shilingi 897 milioni za Tanzania.

Hata hivyo ameachiwa kwa dhamana.

Mkurugenzi wa sasa wa TBC Dk. Ayoub Rioba ameambia BBC kwamba hawezi kuzungumzia taarifa hizo za kufikishwa mahakamani kwa Tido Mhando kwa sasa kwa kuwa "amezisikia pia katika mitandao ya kijamii." Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment

Pages