NA SULEIMAN KASEI
MTANDAO wa Jamii wa
Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita) umetoa mapendekezo manne kwa Serikali
ili kuhakikisha kuwa upotevu wa misitu nchini unadhibitiwa.
Mapendekezo hayo yametolewa
na Ofisa Uraghibishaji wa Miradi Mjumita, Elida Fundi wakati akiwasilisha mada
kwa waandishi wa habari mbalimbali hivi karibuni mwishoni mwa wiki.
Fundi alitaja pendekezo la
kwanza ni kuandaa sera
ambazo zitatambua thamani ya huduma ya mifumoikolojia na mazao ya misitu, hasa
inayohusu maamuzi na mgawanyo wa ardhi.
Alisema pendekezo lingine
ni kupitia sera ili
kuweka uhusiano wa moja kwa moja wa biashara,
misitu na malengo ya kusimamia ardhi yenye misitu.
“Pia sera iunge mkono miradi inayotokana na misitu (mbao,
mkaa) ambayo inanufaisha jamii ili kutoa motisha kwa usimamizi endelevu wa
misitu ya asili; na kufikia mahitaji ya kiuchumi ya mazao ya misitu,” alisema.
Ofisa huyo alisema wakati
umefika kupitia kanuni
ili mazao ya misitu ambayo yamevunwa bila kanuni za usimamizi endelevu
yasihalalishwe kwenye vituo vya ukaguzi.
Aidha Fundi alisema
visababishi vikuu vya upotevu wa misitu upotevu mkubwa wa misitu nchini unasababishwa na
mahitaji makubwa ya ardhi kwa ajili ya kilimo ambapo taarifa ya Naforma ya
mwaka 2015 takribani hekta 372,816 ya misitu hupotea kila mwaka na wakati huo
huo taarifa ya Serikali ya Takwimu zasingi za Hewa Ukaa ya mwaka 2016
inaonyesha hekta 469,000 ya misitu hupotea kila mwaka.
“Taarifa zote mbili zinaonyesha kwamba upotevu huo
umesababishwa ufunguaji wa mashamba kwa ajili ya kilimo,”aliongeza.
Ofisa huyo alisema tafiti za hivi karibuni zinaonyesha
kwamba kati ya asilimia 70 mpaka 80 ya
matukio yaliyosababisha upotevu wa misitu nchini ni ufyekaji wa misitu kwa
ajili ya upanuzi wa mashamba (Kilimo).
Alisema sera zilizopo hazijaweza kutoa muongozo wa
namna ya kutatua kisababishi kikuu cha
upotevu wa misitu nchini akitolea mfano sera ya msitu haina tamko la la sera linalozuia kubadilisha eneo la misitu
kuwa shamba la kilimo, hususani maeneo muhimu ya kiikolojia kwa kuboresha
uratibu na wizara ya kilimo, wizara ya ardhi.
Ofisa Uraghibishaji huyo alisema sera za kilimo
zimekuwa zikihimiza kilimo kikubwa na kidogo bila kuzingatia upotevu wa misitu ya asili na haitoi
fursa kwa jamii na watu binafsi kuanzisha miradi inayotokana na misitu ya asili
iliyosimamiwa kwa uendelevu, ingawa uchumi wa taifa unahitaji mazao
yanayotokana na misitu.
Fundi alisema miradi inayosimamiwa na wananchi ingeleta
motisha kwa jamii na watu binafsi ili wachague kuhifadhi misitu ya asili kwenye
ardhi zao na kusimamia misitu hiyo kutokana na kanuni za usimamizi endelevu.
Alisema upotevu wa misitu umekuwa ukitokea zaidi
katika ardhi za vijiji kwa asilimia ( 45.7 na endapo kiwango cha sasa cha
uharibifu wa misitu kwenye ardhi ya vijiji kitaendelea mpaka kufikia mwaka 2061
hakutakuwepo na misitu kwenye ardhi za vijijiji.
Kwa
upande wake Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG), Bettie
Luwuge alisema pamoja na kuwepo kwa sera nzuri ni jukumu la Serikali kutenga kutengeneza maeneo madogo ya usimamizi wa mkaa ndani ya
misitu katika hifadhi za vijiji kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa endelevu.
Alisema TFCG, Mjumita na Shirika la
Kuendeleza Nishati Tanzania (TaTEDO) kwa ufadhili Shirika la Maendeleo na
Ushirikiano la Uswiss (SDC) wamedhamiria kupigania utunzaji wa misitu na
mazingira kupitia Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS )
hivyo Serikali inapaswa kuunga mkono.
No comments:
Post a Comment