WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma watumie utalaamu wao vizuri na
wafanye kazi kwa uhakika na kwa kujiamini ili matokeo ya utendaji wao
yaonekane.
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Februari 15,
2018) mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Mwanza alipowasili mkoani hapa
kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku saba.
Waziri Mkuu amesema watumishi wa umma wanatakiwa
watumie utalaamu wao vizuri na wafanyekazi kwa kujiamini pamoja na kuwa na
taarifa za kutosha za idara wanazoziongoza ili wananchi waweze kupata tija.
Pia amewataka watendaji kuacha urasimu na
wahakikishe kila fedha iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya
maendeleo inatumika ipasavyo.
"Msimamo wa Serikali ni kuhakikisha
wananchi wanahudumiwa ipasavyo, hivyo watumishi wajiepushe na vitendo vya
rushwa na matumizi mbaya ya fedha za umma."
Pia Waziri Mkuu amewataka watendaji hao wawe
na mpango wa kuwatembelea wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili
hususani za ardhi na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw.
John Mongela alimueleza Waziri Mkuu kwamba atahakikisha wanafanya kazi kwa
bidii na fedha zote za miradi zinatumika kama ilivyokusudiwa.
Hata hivyo Bw. Mongela alizungumza kuhusu hali
ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika mkoa huo kuwa ni ya kuridhisha na
imefikia asilimia 80, pia wameboresha huduma ya mama na mtoto.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, FEBRUARI 15,
2018.
No comments:
Post a Comment