NA SULEIMAN MSUYA
KIJIJI cha Nanjilinji A wilaya ya Kilwa mkoani Mtwara kimefanikiwa
kukusanya zaidi ya shilingi milioni 800, kutokana na utunzaji wa misutu
endelevu.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa Mpingo Conservation and Development Initiative (MCDI),
Jonath Timoth wakati akizungumza na Tanzania Daima ambapo alibainisha kuwa
mikakati yao ni kuona wanavijiji wengi wakiongezeka katika utunzaji wa misitu.
Timoth alisema MCDI imekuwa ikishirikiana na Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania
(TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita)
ikishirikiana kuhakikisha kuwa misitu inakuwa endelevu.
Mkurugenzi huyo alisema kiasi hicho cha fedha kimefanikisha ujenzi
wa nyumba ya kulala wageni yenye vyumba 16, ofisi ya kijiji, madarasa manne na
wanakikundi kunufaika kiuchumi na maendele.
Alisema mikakati yao ni kuendelea kutumia faida ambayo inapatikana
kuboresha huduma za kijamii katika vijiji vilivyopo katika mradi wa utunzaji
misitu pamoja na wanavijiji wenyewe.
Timoth alisema mradi wao unatekelezwa katika vijiji 40, wilaya 8
mikoa minne na matokeo yameonekana kuwa mazuri hali ambayo inawasukuma
kuendelea nao.
“Tupo katika wilaya ya Tunduru ambapo kuna vijiji saba, Kilwa 10,
Rufiji viwili, Liwale 15, Handeni kimoja, Namtumbo viwili, Ruangwa viwili na
Nachingiwea kimoja,” anasema.
Mkurugenzi huyo wa MCDI, alisema kwa sasa wanahifadhi eneo lenye
ukubwa wa hekta 410 na zaidi shilingi bilioni 1.5 zimepatikana kama mapato kwa
kipindi cha miaka sita.
“Pia wakina mama wajawazito
wanapewa 100,000, watoto wakifaulu wanapewa 100,000, tunatoa bima ya afya kwa
wazee, tunatoa chakula shuleni yote haya ni kuhakikisha kuwa utunzaji wa misitu
unakuwa endelevu kwa kile kiinachopatikana kuwarejea watunzaji,” alisema.
Alisema pamoja na kuvuna misitu wamekuwa wakirejesha kwa kuotesha
miti mingine ambapo mwaka jana waliotesha miche 4,000 ya Mkongo, mwaaka huu
wanamiche 10,000 ya Mpingo na Mnungunungu 10,000 ambayo inatajwa kuwa ni miti
inayopotea kwa kasi.
Timoth alisema ili kutunza misitu na kuangalia kuwa unaongezeka au
unapungua wanafanya doria kila mwezi kuangalia misitu isipungue, kuangalia aina
yak wanyamaa kwenye misitu na aina ya ndege ambao wanakuwepo msituni hapo.
No comments:
Post a Comment