Kampuni
ya Bahati Nasibu Tatu Mzuka imekabidhi kalenda 500 kwa Jeshi la Polisi
nchini,kama mwanzo wa uhusiano mwema utakaozaa matunda kati ya Tatu
Mzuka na Jeshi la Polisi.
Akizungumza
na waandishi habari wakati makabidhiano ya kalenda kwa Jeshi la Polisi, Msemaji wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga amesema wameamua
kutengeneza kalenda 500 za Jeshi la Polisi kama sehemu ya kujenga
uhusiano bora, lakini pia kuendeleza kauli mbiu ya Tatu Mzuka ya
ukishinda Tanzania inashinda pia.
Maganga
amesema wao ni raia wema wa Tanzania hivyo ni nafasi ya pekee kuwa
mbele kutokana na kazi ambayo inafanya jeshi la Polisi katika kulinda
watu na mali zao chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP), Simon Sirro,na
kwamba Kauli mbiu ya Tatu Mzuka “Ukishinda Tanzania inashinda”,
“Mchezo
wa bahati nasibu wameweza kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Temeke
katika kusaidia ujenzi wa kituo cha polisi kuwasaidia wananchi wa Mbande
baada ya mapolisi kuuliwa kwa kutokuwa na kituo maeneo ya karibu. "
Tumefanya kitu hiki kwa niaba ya washindi wa mchezo wetu wa bahati
nasibu,ambao mpaka sasa wamefikia idadi ya milioni 6 ambao wote
wamehakikishiwa usalama wao na jeshi la polisi.
Mkuu wa jeshi la Polisi (
IGP ) Simon Sirro ameeleza kuukubali mchezo wa kubahatisha nchini wa
Tatu Mzuka unaoshika kasi kwa kubadilisha maisha ya Watanzania wengi.
IGP
Sirro amesema hayo wakati akipokea kalenda za jeshi hilo
zilizokabidhiwa na viongozi wa Tatu Mzuka kwenye makao makuu ya Jeshi la
Polisi, Posta jijini Dar es Salaam juzi."Mmefanya jambo
jema lakini pia mmeonyesha mfano kwa wengine, binafsi nimeguswa na
mwamko wenu, hongereni sana na endeleeni kuchapa kazi," alisema IGP
Sirro.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akikabidhiwa moja ya Kalenda kati ya 500 zilizotolewa na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Tatu Mzuka,kutoka kwa Mratibu wa Mawasiliano kampuni hiyo Sebastian Maganga (pichani kati).kulia ni Mmoja wa Wakilishi Simon Simalenga.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikabidhiwa moja ya faluna ya Tatu Mzuka kutoka kwa Mratibu wa Mawasiliano Tatu Mzuka, Sebastian Maganga (pichani kati).kulia ni Mmoja wa Wakilishi Simon Simalenga.
No comments:
Post a Comment