HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 24, 2018

Mkurugenzi SBL afanya mazungumzo na maofisa Idara ya Uhamiaji


Dar es Salaam, Machi 23 2018

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie pichani), jana alifanya mazungumzo na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ikiwa ni sehemu ya uboreshaji zaidi wa maslahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

“Tukiwa kama kampuni inayoheshimu sheria na kujali maslahi ya wafanyakazi wetu na nchi kwa ujumla, tumekuwa tukikutana na mamlaka husika ili kuhakikisha haki na maslahi ya wafanyakazi wetu yanalindwa na kuheshimiwa.,” anasema Weesie.
 
SBL imeajiri wafanyakazi zaidi ya 700 katika viwanda vyake vilivyopo Moshi, Mwanza na Dar es Salaam. Bia yake mama ya Serengeti Premium Lager ilizalishwa kwa mara ya kwanza kwa kutumia kimea kwa aslimia 100 na imeweza kushinda zaidi ya tuzo kumi za dhahabu za kitaifa na kimataifa.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002, SBL imekuwa huku ikiongeza idadi ya bidhaa inazozalisha. Baada ya kisisi iikubwa cha hisa kuchukuliwa na Kampuni ya Bia ya AFRIKA Mashariki (EABL)/Diageo mwaka 2010 kumekuwepo uwekezaji mkubwa amboa umefanikisha uzalishaji w3a bidhaa zenye ubora wa kimataifa na kutengeza fursa kwa Watanzania.

Moja kati ya nguzo za Diageo ambayo ni kampuni mama ya SBL ni kujenga na kuwawezesha wafanyakazi wake sehemu yoyote inapofanya kazi ikiwamo Tanzania. Kutokana na hili idadi ya wataalamu wageni imepungua kwa kiasi kikubwa kutoka zaidi ya 30 hadi sita kufikia mwezi Machi 2018 ikiwa ni chini ya asilimia 1 ya nguvu kazi katika kampuni

“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea kuimarisha mahusiano na wafanyakazi wetu. Tutaendelea kukidhi mahitaji yao kwa kuwahakikishia bidhaa bora ikiwa ni sehemu muhimu kwa biashara yetu,”anasema mkurugenzi huyo.

No comments:

Post a Comment

Pages