WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwa amewataka wafanyabiashara wilayani Ruangwa kutumia taasisi za kifedha kukopa
fedha kwa ajili ya kukuza mitaji yao.
Ameyasema hayo leo
(Jumapili, Machi 25, 2018) wakati akizungumza na wafanyabiashara wa wilaya hiyo
katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chama Cha Walimu, wilayani Ruangwa.
Waziri Mkuu ambaye
yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili amesema ni vema
wakatumia taasisi za kifedha zilizopo ili kukuza mitaji yao.
”Naamini sekta ya
biashara ni muhimu katika mabadiliko ya maendeleo, hivyo wafanyabiashara ni
chachu ya maendeleo kokote na Serikali itaendelea kuwaunga mkono.”
Amesema katika
kuhakikisha riba zinapungua, Rais Dkt. John Magufuli anaendelea kuzungumza na wamiliki
wa taasisi za kifedha ili waone namna ya kupunguza riba hiyo.
Waziri Mkuu amesema
lengo la Serikali la kuchukua hatua hiyo ni katika kutekeleza mkakati wake wa kuwawezesha wafanyabiashara ili waweze kupata
mikopo yenye riba nafuu.
Pia Waziri
Mkuu amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali ipo pamoja nao na imedhamilia
kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama maji na afya.
Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa
Wafanyabiashara wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Said Shea amewaomba wafanyabiashara
wenzake watumie fursa za maendeleo zilizoko wilayani humo kwa kupanua wigo wa
biashara zao.
IMETOLEWA NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI,
MACHI 25, 2018.
No comments:
Post a Comment