HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 20, 2018

Mashindano ya EAAR yapigwa kalenda

NA MWANDISHI WETU, KARATU

MASHINDANO ya riadha kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 18 ya Kanda ya Tano ya Afrika (EAAR), yaliyopangwa kufanyika nchini Mei 4-5, yameahishwa.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday alisema mjini hapa jana kwamba mashindano hayo sasa yatafanyika kuanzia Mei 12-13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Alisema nchi wanachama zimeomba kusogezwa mbele kwa mashindano hayo na Jumatano ijayokutakuwa na mkutano wa Kamati ya Ufundi kupanga tarehe ya kuanza kwa kambi ya timu hiyo ya vijana na mambo mengine.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya RT, Robert Kalyahe alisema jana kwa njia ya simu kuwa, kwa sasa wachezaji wanafanya mazoezi katika kanda zao kabla ya kukusanywa pamoja katika tarehe itakayopangwa Jumatano jijini Dar es Salaam.

Tanzania mwaka jana iliandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Kenya iliyoshika nafasi ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

Pages