HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 26, 2018

WAZIRI MKUU AMJULIA HALI BW. ABBAS KANDORO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Bw. Abbas Kandoro ambaye amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu.

Akiwa hospitalini hapo leo (Jumatano, Aprili 25, 2018), Waziri Mkuu amefarijika baada ya kumkuta Bw. Kandoro na wagonjwa wengine waliolazwa kwenye hospitali hiyo wakihudumiwa vizuri.

Pia Waziri Mkuu amemjulia hali Mbunge wa Viti Malumu (CUF) Bi. Shamsiha Azizi Mtambo ambaye amelazwa katika ya Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU)kwenye
hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa hao na kuwaeleza kwamba madaktari wataendelea kuwahudumia vizuri ili kuhakikishia afya zao zinaimarika na kurejea katika shughuli zao za kila siku.

Kwa upande wake, Bw. Kandoro alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kumjulia hali, pia aliwashukuru madaktari na wauguzi wa h
ospitali hiyokwa huduma nzuri wanazompatia tangu alipofika hospitalini hapo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMATANO, APRILI 25, 2018.

No comments:

Post a Comment

Pages