HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 26, 2018

NSSF YAWAELIMISHA WAAJIRI KUHUSU SHERIA MPYA YA HIFADHI YA JAMII NA WAJIBU WAO ILI KULINDA HAKI ZA WANACHAMA

Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF, Bathow Mmuni,  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa Semina ya Waajiri kuhusu Sheria Mpya ya Hifadhi ya Jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na NSSF.
Baadhi ya waajiri katika semina hiyo.

Meneja  Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke, James Oigo, akisisitiza jambo wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na NSSF. Kulia ni Kaimu Meneja Kiongozi NSSF Mkoa wa Ilala, Christine Kamuzora na Kaimu Meneja Bima ya Afya NSSF, Zakia Mohamed.
Kaimu Meneja Bima ya Afya NSSF, Zakia Mohamed, akizungumza wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na NSSF. 
Kaimu Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Kimaro, akizungumza wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi na kuandaliwa na NSSF. 
Meneja  Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke, James Oigo, akitoa mada wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi na kuandaliwa na NSSF. 
Baadhi ya Waajiri wakiwa katika semina.
Meneja  Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke, James Oigo, akijibu maswali wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi na kuandaliwa na NSSF. Kushoto ni Meneja Kiongozi NSSF Mkoa wa Kinondoni,Marko Mgheke na Kaimu Meneja wa Uendeshaji NSSF, Omary Mzia.

NA MWANDISHI WETU

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeendesha semina kwa waajiri  wa Mkoa wa Temeke katika jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na waajiri takrabani 200 waliopo katika mkoa wa Temeke  kwa mgawanyo wa mipaka ya NSSF.


Akifungua Semina hiyo juzi, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bathow Mmuni, aliwaambia waajiri kwamba sheria mpya ya hifadhi ya jamii imeshasainiwa na Rais na sasa zimebakia taratibu za kiuendeshaji.

‘Semina hizo ambazo zimepangwa kuendelea nchi nzima zikiwa na lango la kuwahimiza waajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati ili kuliwezesha Shirika kulipa mafao ya wanachama kwa ufanisi, kuzijua changamoto zinazowakumba waajiri na kujibu hoja nyingi walizokuwa nazo waajiri kuhusu uelekeo mpya baada ya Mifuko ya Hifadhi ya jamii kuunganishwa na kubaki miwili yaani NSSF na PSSSF’, alisema Mmuni.


Naye Meneja  Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke, James Oigo, akiwasilisha mada kwa waajiri hao alisema, Sheria mpya imefafanua kuwa Mfuko mpya wa waajiriwa wa sekta ya Umma (PSSSF) utakuwa unahudumia waajiriwa wote waliopo katika sekta ya umma wakati NSSF itahudumia waajiriwa wote wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.

Akifafanua kuhusu Sheria hiyo Oigo alisema kuwa, NSSF ni mfuko pekee utakaokuwa unahudumia wanachama Waajiriwa wote wa sekta binafsi, Waajiriwa wote wa Kigeni walioajiriwa Tanzania Bara, Waaajiriwa wote waliajiriwa katika taasisi za kimataifa zinazofanya kazi Tanzania Bara, Watu wote waliojiajiri wenyewe na wale wa sekta isiyo rasmi.

Aidha  amefafanua kuwa,waajiriwa wote ambao wataajiriwa baada ya sheria hii kuanza ndio watakuwa katika mfuko ama wa PSSSF endapo wanaajiriwa katika sekta ya umma na NSSF endapo wanaajiriwa katika sekta binafsi, Aidha kwa  wale ambao walishaajiriwa wakati sheria hii inaanza  ambapo walikuwa katika mifuko iliyounganishwa watakuwa wanachama wa mfuko wa PSSSF bila kujali wapo setka binafsi au ya umma na wale ambao walikuwa wanachama wa NSSF watabakia kuwa wanachama wa NSSF bila kujali sekta wanayotoka. Alizidi kufafanua kuwa  kanuni ya ulipaji mafao na idadi ya mafao yatakuwa ya aina moja kwa mifuko yote miwili.

Wakati huo huo, Meneja wa NSSF Mkoa wa Kinondoni,  Marco Magheke,   alisema, Shirika limejipanga kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wanachama wake na kuwahakikishia waajiri kuwa NSSF itamaliza changamoto ndogondogo ambazo waajiri walizitaja wakati wa semina hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages