Kamati
ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi
katika kikao chake kilichopita ilipitia taarifa na matukio mbalimbali na
kufanya uamuzi ufuatao;
Mechi namba 171 (Njombe
Mji 0 vs Simba 2). Klabu
ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuonyesha
vitendo vinavyoashiria ushirikina katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 3, 2018
kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, ikiwemo pia mshabiki mmoja wa timu hiyo
kuingia uwanjani na kuchukua taulo la kipa wa Njombe Mji lililokuwa golini.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu
Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 165
(Mtibwa Sugar 0 vs Simba 1). Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh.
500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani baada ya
filimbi ya mwisho ya mechi hiyo iliyofanyika Aprili 9, 2018 kwenye Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro.
Kitendo
hicho cha washabiki wa Simba iliyokuwa ikicheza ugenini ni ukiukaji wa Kanuni
ya 14(11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, wakati adhabu dhidi yao
imezingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 177
(Singida United 0 vs Mtibwa Sugar 3). Mchezaji Tafadzwa Kutinyu wa Singida
United amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana
na kufanya vitendo vyenye kuonyesha imani za ushirikina katika mechi hiyo
iliyochezwa Aprili 6, 2018 kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Katika
mchezo huo, Kutinyu alichukua taulo la kipa wa Mtibwa Sugar na kulirusha
jukwaani kwa washabiki wa Singida United ambao waliondoka nalo. Adhabu dhidi
yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 37(7) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa
Wachezaji.
Mechi namba 184 (Mbao
0 vs Lipuli 0).
Klabu ya Mbao imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na mshabiki
wake kuingia uwanjani na kuchukua glovu za akiba za kipa wa Lipuli zilizowekwa golini na kukimbia
nazo, kitendo kinachoonyesha imani za kishirikina.
Adhabu
dhidi ya Mbao katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 6, 2018 kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu
kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 185 (Yanga
1 vs Singida United 1). Klabu ya Singida United imepigwa faini
ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani
katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 11, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kitendo
hicho ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na
adhabu dhidi ya klabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu
Taratibu za Mchezo.
Vilevile
Bodi ya Ligi imepeleka malalamiko kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) dhidi ya Meneja wa Singida United, Ibrahim
Mohamed kwa kuongoza vurugu za timu yake kulazimisha kuingia uwanjani kwa kutumia
mlango usio rasmi.
Mechi namba 191
(Simba 3 vs Mbeya City 1). Klabu ya Simba imepewa Onyo Kali
kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika sita katika mechi
hiyo iliyofanyika Aprili 12, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kitendo
cha Simba ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo
wakati adhabu dhidi yao imekijita katika Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu
Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 194 (Azam
0 vs Njombe Mji 1).
Kocha wa Azam, Aristica Cioba amesimamishwa hadi suala lake la kumtukuna
Mwamuzi baada ya mechi kumalizika litakaposikilishwa na Kamati ya Nidhamu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Uamuzi wa kumsimamisha umefanywa
kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi.
Kabla
ya kumtukana Mwamuzi, Kocha huyo aliondolewa kwenye benchi (ordered off) kwa
kupinga maamuzi kwa maneno na vitendo katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 15, 2018
katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mechi namba 200
(Simba 2 vs Tanzania Prisons). Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh.
500,000 (laki tano) kutokana na kuwakilishwa na maofisa watatu badala ya wane kwenye kikao cha
maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili
16, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kitendo
chao ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(2a) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na
adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu
Taratibu za Mchezo.
IMETOLEWA NA BODI YA LIGI KUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment