Mmiliki wa Kampuni ya Danaos, Ali Mzee Yusouf, akiwa katika picha ya pamoja na mabaharia wa
Tanzania huku wakiwa wameshika fulana maalumu
ambayo waliweka saini ya kupiga vita dawa za kulevya kwa kupitia kampuni yao. Hafla hiyo ilifanyika Chukwani
Zanzibar. (Picha na Talib Ussi).
Na Talib Ussi, Zanzibar
Na Talib Ussi, Zanzibar
Mmiliki wa Kampuni ya
Danaos ambayo inamiliki chuo cha mabahari Zanzibar Ali Mzee Yusouf amesema kuwa idadi ya mabahari
wanaofanyakazi katika meli duniani kutoka Zanzibar imeshuka kutoka 1000 hadi
200 kutokana na baadhi kukamatwa na usafirishaji wa dawa za kulevya.
Yusouf aliyazungumza
hayo huko katika chuo cha Mabaharia Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar
wakati wakizindua tamko maalumu la kupinga usafirishaji wa madawa ya kulevya
kupitia mabaharia wa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla wake.
“Usafirishaji wa dawa za kulevya umetushushia hadhi yetu kwani kampuni yetu ilikuwa inaminiwa duniani
kote lakini sasa tunaona athari yake” alieleza Mzee Yusouf.
Alieleza kuwa zaidi ya
mabahari saba (7) wamekamatwa wakiwa na madawa ya kulevya wakiwa safarini mara
nyingi kutoka Brazil kuelekea bara la Ulaya.
Akizungumza katika
shughuli hiyo Mwanasheria ya kampuni hiyo Abdallah Juma Muhammed alisema
kutokana na wingi wa usafirishaji wa madawa hayo, imeundwa sheria kama
Mtanzania mmoja akikutwa na madawa na Watanzania wote wanashushwa katika meli.
Kutokana na hali hiyo
aliwaomba mabaharia walikuwepo hapo katika tukio hilo kujitambua wanalokwendea
na kuwajingiza katika majanga ambayo hupoteza taaswira ya maisha yao.
“Tunajua soote tunapokwenda
ubaharia familia zetu zoote zinategemea manufaa lakini jee tukikamatwa na
madawa nikwamba mfumo mzima wa maisha ya familia tumeua baada ya kututegemea
sasa tutawatia matatizo” alieleza Mwanasheria huyo.
Alisema kila kepteni wa
meli ya nje sasa hivi anakataa kupokea mabaharia kutoka Tanzania kutokana na
uharamia huu ambao umeingia wa kusafirisha madawa ya kulevya.
Sambamba na hilo
aliwataka mabaharia woote kutoka Tanzania kuwa askari kwa ajili ya kulijengee
taifa taaswiraa bora ili matukio hayo kwa watanzania yasitokee tenna.
Kwa upande wake Kepten
Stelios Petronions ambaye ni mwalimu wa chuo cha mabaharia Zanzibar (ZDMMI)
alieleza kuwa mtandao wa kusafirisha madawa ya kulevyo ni mkubwa na unambinu
nyingi na kuwataka mabaharia wa Tanzania wasiwe rahisi kuhadalika usafirishaji
wa madawa ya kulevya.
“Hawa mabwana ambao
wanafanyabiashara hii wananguvu na wanakila uwezo kwa hiyo tnakazi ngumu ya
kupambana nao lakini tukishirikiana makepteni na Mabaharia kwa ujumala tunaweza
kuhimili kama sikushinda kabisa” alieleza Kepteni huyo.
Aliwaambia mabaharia
kabla ya kujibu chochote mtu anapopokea ujumbe kutoka kwa waharamia hao ni
vyema akafuata taratibu usalama ili asijeakajiingiza katika majanga.
Naye Mwakili wa Mamlaka
ya Usafirini Baharini Zanzibar khamis Mhummed Ali aliwaomba mabaharia hao
kuacha kazi hiyo kwa kufanyakazi hiyo ni kupoteza taaswira ya Taifa.
“Tusiwe na utajiri wa
haraka kwani tunaweza hata tukapoteza maisha yetu” alieleza Ali.
Alieleza kuwa ni vijana
wangapi leo wanapoteza ajira hiyo kutokana wenzao kukutwa na madawa na
kushushwa na huku wengine wakisalia jela katika nchi mbali mbali duniani
ikiwemo Brazili, Itali na Morishiaz.
“Hawa wauzaji ni
wajanja sana, wanaweza kukupa mzigo mara moja hadi mbili lakini mara ya tatu
wao wanakukamatisha kwani lengo lao ni kukuharibia” alileza Ali ambaye ni
Mkaguzi wa Meli.
No comments:
Post a Comment