Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) limewaondoa Waamuzi
wawili kwenye orodha ya Waamuzi wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoendelea
kwenye vituo vinne vya Geita,Singida,Rukwa na Kilimanjaro.
Waamuzi
walioondolewa katika orodha hiyo ni Seleman Nonga kutoka Arusha aliyekuwa
katika kituo cha Geita na Dadu Fadhil Msemo wa Kilimanjaro aliyekuwa kituo cha
Singida.
Nonga
ameondolewa baada ya kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji ,kushindwa kumudu
mchezo,kukosa umakini,kutozingatia sheria ipasavyo kwa kipindi kikubwa cha
mchezo na kupata alama ndogo katika tathmini ya Wasimamizi kwenye mchezo namba
A7 kati ya Kumuyange FC dhidi ya Ambassador.
Msemo
ameondolewa baada ya kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji ,kushindwa kumudu
mchezo,kukosa umakini,kutozingatia sheria ipasavyo kwa kipindi kikubwa cha
mchezo na kupata alama ndogo katika tathmini ya Wasimamizi kwenye mchezo namba
C6 kati ya Temeke Squad dhidi ya Mtwivila City.
Waamuzi
hao wawili wanatakiwa kuondoka kwenye vituo vya Geita na Singida leo Jumamosi
Mei 12,2018.
Cliford
Mario Ndimbo
Afisa
Habari na Mawasiliano TFF
Mei 12,2018
No comments:
Post a Comment