Kamati
ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa) katika kikao chake cha Mei 1,
2018 chini ya Mwenyekiti wake Bw. Clement Sanga ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi
Kuu ya Vodacom, na malalamiko ya klabu za Yanga na Arusha FC na kuyafanyia uamuzi.
Kamati imekataa malalamiko ya Yanga kutaka ipatiwe ushindi wa pointi tatu na mabao matatu dhidi ya Mbeya City kwa timu hiyo kuwa na mchezaji zaidi kwenye mechi, kwa vile hakuna Kanuni yoyote ya Ligi Kuu inayoweza kubadili matokeo ya uwanjani kwa mazingira hayo.
Kamati imekataa malalamiko ya Yanga kutaka ipatiwe ushindi wa pointi tatu na mabao matatu dhidi ya Mbeya City kwa timu hiyo kuwa na mchezaji zaidi kwenye mechi, kwa vile hakuna Kanuni yoyote ya Ligi Kuu inayoweza kubadili matokeo ya uwanjani kwa mazingira hayo.
Hakuna
namna yoyote ile mchezaji anayezidi (extra player) kubadili matokeo ya mchezo.
Katika mazingira ya extra player likifungwa bao, Mwamuzi atalikataa bao hilo. Kutokana
na kanuni za Ligi kutojitosheleza katika suala hilo la extra player, Kamati iliangalia
Kanuni za FIFA na kufikia uamuzi huo.
Mchezaji
Ramadhan Malima wa Mbeya City ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu, lakini
akatoka kwenye chumba cha kuvalia (dressing room) kwenda kushangilia bao la
kusawazisha la timu yake amesimamishwa hadi suala lake litakaposikilizwa na Kamati
ya Nidhamu TFF. Uamuzi wa kumsimamisha umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu
kuhusu Usimamizi wa Ligi.
Kwa
upande wa waamuzi, kulikuwa na upungufu katika suala la kusimamia ubadilishaji wa
wachezaji (substitution), hivyo Kamati ya Waamuzi ya TFF imeandikiwa barua ili
ichukua hatua dhidi ya wahusika.
Kamati
ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa) katika kikao chake cha Mei 1,
2018 chini ya Mwenyekiti wake Bw. Clement Sanga ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi
Kuu ya Vodacom, na malalamiko ya klabu za Yanga na Arusha FC na kuyafanyia uamuzi.
Mechi
namba 199 (Mbeya City 1 vs Yanga 1). Klabu ya Mbeya City imepigwa faini ya sh.
500,000 (laki tano) kutokana na vurugu za washabiki wake ikiwemo kurusha mawe
na chupa uwanjani katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 22, 2018 kwenye Uwanja
wa Sokoine jijini Mbeya. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1)
ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Kwa
vile mchezaji Obrey Chirwa wa Yanga alionywa kwa kadi ya njano kwa kosa la
kumsukuma mchezaji wa Mbeya City ingawa kwenye picha za televisheni inaonekana
kama alipiga kiwiko, Kamati haikutoa adhabu nyingine kwa vile tayari
ameadhibiwa.
Hata
hivyo, klabu ya Yanga imeandikiwa barua kuhusu kumuonya mchezaji huyo kwa vile
kumbukumbu zinaonyesha ameshafanya matukio ya utovu wa nidhamu mara kadhaa akiwa
uwanjani.
Mechi
namba 178 (Simba 1 vs Yanga 0). Mchezaji Kelvin Yondani wa Yanga amesimamishwa
hadi suala lake la kumtemea mate Asante Kwasi wa Simba katika mechi hiyo iliyochezwa
Aprili 29, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam litakaposikilizwa na
Kamati ya Nidhamu ya TFF.
Adhabu
ya kusimamishwa imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu
Usimamizi wa Ligi.
Mkuu
wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amepewa Onyo Kali kwa
kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake baada ya mchezo kumalizika.
Kitendo chake ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14(11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za
Mchezo, na adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi
Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
MALALAMIKO YA ARUSHA
FC
Kamati
imeipa Arusha FC ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya African Sports
kuchezesha wachezaji wawili waliotumia leseni za kughushi (non qualified) katika
mechi ya Kundi B Ligi Daraja la Pili (SDL) kati ya timu hizo iliyochezwa Uwanja
wa Mkwakwani jijini Tanga.
Uamuzi
huo dhidi ya African Sports umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(17) na 42(23)
za Ligi Daraja la Pili. Nayo Arusha FC imepewa ushindi kwa kuzingatia Kanuni ya
14(36) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.
Vilevile
viongozi wa African Sports waliohusika kughushi leseni zilizotumiwa na
wachezaji hao ambao hawakusajiliwa watafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya TFF
kwa ajili ya hatua zaidi.
IMETOLEWA NA BODI YA LIGI
KUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment