*Yasema maitosita kumuondoa mwendeshaji wa sasa
SERIKALI imesema inakusudia kuongeza mtoa huduma mwingine katika uendeshaji wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) ambayeataingiza mabasi yake na kutathmini ufanisi wa mbia wa sasa ili kuimarisha huduma ya usafiri Jijini Dar es salaam .
Amesema iwapo itabainika kwamba mwendeshaji wa sasa ana matatizo yaliyokithiri, Serikali haitasita kumuondoa na kumpa mwendeshaji mwingine kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kwa uhakika.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo (Alhamisi, Mei 10, 2018) wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Bw.Maulid Mtulya katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.
Katika swali lake Bw. Mtulia alitaka kupata kauli ya Serikali juu ya uboreshaji wa wa
mradi wa UDART unaotoa huduma ya usafirishaji wa abiria Jijini Dar Es
Salaam ili kuweza kuwaondolea wananchi changamoto ya usafiri.
“Tunatafuta
mbia mwingine aweze kuingiza mabasi yake kwenye mradi huu ili aweze
kuongeza ushindani na nasi tupate kupata huduma bora kwa maana ya
ushindani utaongeza huduma bora zaidi,” amesisitiza.
Waziri Mkuu ameongeza kuwawako
wawekezaji wa ndani na nje ukiwemo Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar Es
Salaam (UWADAR) ambao wameonyesha nia na uwezo wa kutoa huduma hiyo na
kuufanya mradi huo kutoa huduma kwa ubora unaotakiwa.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu, amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote
nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri suala la usafi wa mazingira katika
maeneo yao la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
“Mheshimiwa
Spika Kupitia Bunge lako tukufu, nawaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi
pamoja na Maafisa Afya wasimamie zoezi la usafi na kuboresha
miundombinu yote na utawapima kupitia zoezi hili,” amesema.
Amesema
hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni
aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kutatua tatizo la usafi wa
mazingira pamoja na miundombinu hususani katika masoko hali ya kuwa
Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakusanya fedha nyingi bila
kuboresha maeneo na kukithiri kwa uchafu.
Waziri
Mkuu amesema suala la usafi limekuwa likifanyika kila jumamosi ya
mwisho wa mwezi baada ya kuasisiwa na Rais Dkt. John Magufuli, hivyo
ametumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji hao wahakikishe maeneo yao
yanakuwa safi na miundombinu inayoweza kutumika wakati wote.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
ALHAMISI, Mei 10, 2018.
No comments:
Post a Comment