Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza
jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Edmund
Mndolwa mara baada ya kuwasili katika chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole
Bagamoyo mkoani Pwani. Rais huyo wa Zimbabwe alisoma Shuleni hapo mwaka 1963
pamoja na wapigani Uhuru wa Chama cha FRELIMO na ilijulikana kama Shule ya
Mafunzo ya Ufundi ya wapigania Uhuru wa Chama
cha FRELIMO.
Rais wa
Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza na wafanyakazi pamoja na wanafunzi
wanaosoma katika Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole ambapo miaka ya nyuma
alisoma hapo wakati huo ikijulikana kama Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani
Uhuru ya Chama cha FRELIMO.
Rais wa
Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiangalia moja ya sufuria waliokuwa wakiitumia
katika matumizi yao ya kila siku wakati
wakisoma katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha
FRELIMO.
Rais wa
Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiwa katika picha na Waziri wa Katiba na Sheria
Profesa Palamagamba Kabudi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha
Mapinduzi CCM Dkt. Edmund Mndolwa, Viongozi wengine wa Tanzania na Zimbabwe
pamoja na wanafunzi wanaosoma katika chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole
Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa
Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo wakati alipokuwa akielekea katika moja ya madarasa ambayo walikuwa
wakiyatumia kuanzia mwaka 1963.
Rais wa
Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitoka katika moja ya mabweni waliyoyatumia katika
mwaka 1963 wakatika wakiwa katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru
ya Chama cha FRELIMO ambacho sasa kina julikana kama chuo cha Kilimo na Mifugo
cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa
Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Profesa
Palamagamba Kabudi mara baada ya kumaliza kukagua baadhi ya madarasa na mabweni
waliyokuwa wakiyatumia katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya
Chama cha FRELIMO ambacho sasa kinajulikana kama chuo cha Kilimo na Mifugo cha
Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa
Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akipunga mkono kwa kikundi cha ngoma za asili
wakati akiondoka katika eneo la chuo hicho cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani. PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment