HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 01, 2018

BISKUTI ZA QUEEN COOKIES KUONDOA CHANGAMOTO YA MAMA KUKOSA MAZIWA YA KUNYONYESHA

 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe  Irene Isibika akionyesha Biskuti zinazoitwa Queen Cookis ambazo ni maalum kwa kutoa maziwa  kwa akina mama wanaonyenyesha ambao maziwa yao hayatoki kwa wingi na kusababisha mototo kutoshiba vizuri.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe  Irene Isibika akiwaonyesha wananchi waliotembelea katika banda la Chuo Kikuu cha  Mzumbe  Biskuti zinazoitwa Queen Cookis ambazo ni maalum kwa kutoa maziwa  kwa akina mama wanaonyenyesha.
.....................................................................................

BISKUTI zinazoitwa Queen Cookis zinaelezwa ndio mkombozi na suluhu kwa akina mama wanaonyenyesha ambao maziwa yao hayatoki kwa wingi na kusababisha mototo kutoshiba vizuri.

Imeelezwa biskuti hizo ambazo zimebuniwa na wahadhiri hao baada ya kufanya utafiti wa kisayansi  bado hazijaanza kuuzwa rasmi kwani mchakato unaoendelea ni kuzisajili na kupata vibali vya mamlaka husika.

Akizungumza kwenye banda la Chuo kikuu cha Mzumbe lililopo kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Mhadhiri wa Chuo hicho Irene Isibika amesema biskuti hizo zinaongeza maziwa ya mama anayenyonyesha.

“Biskuti hizi tunaamini baada ya kuingia sokoni rasmi zitamaliza tatizo la akina mama wengi wanaonyonyesha kulalamika maziwa kutotoka kwa wingi.Ni biskuti ambazo mlaji mbali ya kupata ladha anaongeza maziwa na hivyo anaponyonyesha mototo ana uhakika wa kushiba.

Isibika anasema kuwa biskuti hizo kwa mtuamiaji anaweza kula biskuti mbili kwa siku na zikatosha kabisa kumfanya kuwa na maziwa ya kutosha.

Pia mbali ya kumfanya mama kuwa na maziwa mengi , yanasaidia pia kukuza akili za mototo mchanga na hivyo kwa mtumiaji hupata faida zaidi ya moja.

“Tunachofurahia zaidi mama anayenyonyesha hatakuwa na muda tena wa kubeba chupa ya chai kwa ajili ya kuweka uji ili anywe na kupata maziwa.

“Atabeba biskuti yake na kisha atakula wakati wowote.Tumeamua kumrahisisha mama anayenyonyesha kutoafikiria ale nini awe na maziwa ya kutosha,”amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages