NAMWANDISHI WETU, SONGEA
WAENDESHA
Baiskeli kutoka Mkoa wa Simiyu wameng’ara katika mashindano ya Baiskeli
yaliyoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Songea Mississippi (SOMI),
kupitia Tamasha la Majimaji Selebuka.
Mashindano hayo
ya Baiskeli ya Kilomita 100 kutoka MbingaMjini hadi Uwanja wa Majimaji mjini
Songea Mkoa wa Ruvuma, Masunda Duba akitumia baiskeli ya kawaida huku pia akiwa
hana vifaa maalumu vya mchezo huo kama vile jezi, kofia ngumu na viatu
aliwafunika wenzake ambao walikuwa na vifaa vya kisasa baada ya kushinda
akitumia saa 2:53.05.
Duba
alifuatiwa na mwenzake kutoka Simiyu, Boniphace Masunda aliyetumia saa 2:54.21
huku nafasi ya tatu ikienda kwa Ipyana Mbogela kutoka Iringa aliyetumia saa
3:06.55.
Nafasi ya
nne ilikwenda kwa Ombeni Mbilinyi pia kutoka Iringa aliyetumika saa 3:06.58
huku mshindi wa tano akiwa ni Oscar Kayombo wa Songea aliyetumia saa 3:20.53.
Mshindi wa
sita aliibuka Aso Gadas kutoka Dar es Salaam aliyetumia saa 3:28.17, nafasi ya
saba Samir Rashid pia wa Dar es Salaam saa 3:29.46, nafasi ya nane Hagai Sanga
wa Mbeya saa 3:34.01 huku nafasi ya tisa ikienda kwa Elias Zawadi pia wa Mbeya
saa 3:47.13.
Bingwa
mbali ya kuzawadiwa Kombe aliondoka na kitita cha Sh. 500,000 mshindi wa pili Sh.
300,000 na wa tatu Sh. 200,000 na kutafutiwa mashindano nje ya nchi huku pia mchezaji
kutoka mjini Songea, Oscar Kayombo atapata nafasi ya kutafutiwa mashindano nje
ya nchi.
Akizungumzia
siriya ushindi, Masunda alisema mchezo wa baiskeli kigezo si baiskeli bali mazoezi,
Tamasha la
Majimaji Selebuka ambalo lilianza Julai 14 kwa shughuli mbalimbali ikiwamo
maonyesho ya Wajasiriliamali, Utalii wa Ndani, Mdahalo kwa Wanafunzi, Ngoma za
Asili, Riadha, Mpira wa Miguu na Riadha litafikia tamati leo kwa mechi ya
kukata na shoka kati ya Simba Veterani na Yanga Veterani kwenye dimba la
Majimaji ambako kiingilio ni Sh. 2,000.
No comments:
Post a Comment