Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Umma
kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Kituo cha Kizumbi mjini
Shinyanga, Julai 14, 2018. (Plicha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Chuo cha Ushirika
Moshi, Kituo cha Kizumbi mjini Shinyanga, Julai 14, 2018. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
“Ninawapongeza wazawa walioamua kujenga
kiwanda hiki kwa sababu viwanda kama hivi vinasaidia kukuza kilimo hapa nchini,
kiwanda hiki kinachambua pamba na kusindika mafuta,” alisema.
Ametoa pongezi hizo jana jioni (Ijumaa,
Julai 13, 2018) wakati akizungumza na
wafanyakazi wa kampuni ya GAKI Investment pamoja na wananchi waliofika
kumsikiliza mara baada ya kukagua utendaji kazi wa kiwanda hicho kilichopo
Manispaa ya Shinyanga.
Waziri Mkuu alisema amevutiwa na ujenzi wa kiwanda
hicho kwa sababu kinatoa uhakika wa soko la pamba ikizingatiwa kwamba mikoa
yote inayolima zao hilo, mwaka huu imezalisha pamba kwa wingi kuliko kawaida.
“Mwitikio wa wakulima wa zao la pamba unaonyesha
kwamba bado wana imani na Serikali yao na ndiyo maana nimewaonya wajumbe wa
bodi ya SHIRECU kuwa wajihoji kama kweli wameomba nafasi hizo ili kuwatumikia
wananchi,” alisema.
“Msije mkadhani kuwa SHIRECU ni mahali pa kuganga
njaa. La hasha! Ni mahali pa kukuza soko la pamba. Tunataka viongozi wa sasa watambue
kuwa hawajaenda SHIRECU ili kushiba, lazima walete mabadiliko kwenye ushirika
na kama hawawezi waachie ngazi,” alisisitiza.
Aliwataka watumishi wa kiwanda hicho wafanye kazi
kwa uaminifu na watunze mashine za kiwanda hicho ili kiweze kufanya kazi kwa
muda mrefu.
Mapema, akitoa
maelezo ya uzalishaji wa kiwanda hicho kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa
GAKI Investment, Bw. Gaspar Kileo alisema
kampuni hiyo inajishughulisha na ununuzi wa pamba kutoka mikoa ya Shinyanga,
Simiyu na Tabora.
Alisema uchambuzi wa pamba kwenye kiwanda
hicho unatumia mashine zenye uwezo wa kuzalisha marobota 400 kwa siku. “Hapa
kiwandani pia tunakamua mafuta yatokanayo na mbegu za pamba na tuna uwezo wa kuzalisha
lita 10,000 kwa siku,” alisema.
Alisema ili kuunga mkono kaulimbinu ya
Tanzania ya viwanda, kampuni hiyo imeamua kujenga kiwanda kingine cha kuchambua
pamba wilayani Meatu.
Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake wilayani
Shinyanga kwa kukagua shughuli za maendeleo na kuzungumza na wananchi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JULAI 14, 2018.
No comments:
Post a Comment