WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania bado inawahitaji wawekezaji zaidi
katika sekta ya uzalishaji wa sukari ili iweze kukidhi mahitaji.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Mauritius nchini Tanzaniamwenye makazi yake Maputo nchini Msumbiji,
Mheshimiwa Jean Pierre Jhumun, ofisini kwake jijini Dodoma.
“Mwaka
jana nilikiwa nchini Mauritius nilihudhuria Jukwaa la Wafanyabiashara
na Wawekezaji kati ya Tanzania na Mauritius, ambapo nilipata fursa ya
kuwashawishi wawekezaji wa Mauritius waje kuwekeza kwenye viwanda vya
sukari nchini,”.
Ameongeza
kuwa Tanzania ina fursa kubwa ya maeneo ya uzalishaji wa sukari ambayo
bado hayajaendelezwa, hivyo kama kuna wawekezaji walio tayari na
wamekidhi vigezo waendelee na hatua za uzalishaji.
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa mbali na kuhitaji wawekezaji kwenye sekta ya
sukari, pia amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Mauritius kuja
kuwekeza kwenye sekta ya uvuvi. “Mnaweza
kuja kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji wa samaki kwani tuna
bahari, mito na maziwa yenye samaki wa aina mbalimbali,”
Kwa upande wake,
Balozi Jhumun amesema wawekezaji wa Mauritius wapo tayari kuwekeza
katika uzalishaji wa sukari pamoja na uvuvi na wameshafanya utafiti
katika baadhi ya maeneo.
Balozi
Jhumun amesema ameambatana na Mwenyekiti wa Mfuko wa Uwekezaji wa
Sukari, Bw. Gansam Boodram kutoka nchini Mauritius kwa ajili ya
kufuatilia maeneo ya uwekezaji.
“Tumeitikia
wito wa Rais Dkt. John Magufuli wa kututaka kusaidia katika
upatikanaji wa wawekezaji watakaokuja Tanzania kuwekeza kwenye viwanda
vya uzalishaji wa sukari,”.
Naye Bw.
Boodram amesema tayari wameshatembelea baadhi ya maeneo wanayohitahi
kwa ajili ya uwekezaji na wameshafanya utafiti wa udongo pamoja na
masoko. Maeneo waliyoyafanyia utafiti ni Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma
pamoja na Rufiji mkoani Pwani.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, AGOSTI 15, 2018.
No comments:
Post a Comment