Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse, akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma tatu kwa mpigo za Benki ya NMB ikiwemo kufungua akaunti kwa njia ya simu. Hafla hiyo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa huduma mpya za benki hiyo.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi huo.
Mgeni rasmi Naibu Gavana wa Benki Kuu (BoT), Bernard Kibesse (tai nyekundu katikati), akiwa katika picha ya pamoja.
Na MWANDISHI WETU
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imepongeza mfumo wa mabadiliko ya kidijitali unaoendelea kuboreshwa katika Benki yak NMB, huku ikiahidi kusapoti mapinduzi hayo ya kimfumo ili kupunguza idadi ya Watanzania wasiotumia huduma za kibenki.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Gavana wa BoT, Dk. Bernard Kibesse, wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma tatu kwa mpigo uliofanywa na Benki ya NMB jana, ikiwemo ya ufunguaji wa akaunti ya benki kwa kutumia simu ya mkononi.
Uzinduzi huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Naibu Gavana Kibesse, ambako pamoja na ufuanguaji wa akaunti, pia alizindua App mpya iitwayo NMB Klik na NMB Scan Pay, ikiwa ni muendelezo wa maboresho ya kidijitali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Gavana Kibesse alisema kwamba mchakato wa kuipeleka Tanzania katika Uchumi wa Kati unahitaji ubunifu wa kihuduma hususani kwa taasisi na kifedha na kwamba katika hilo NMB imejipambananua.
Alibainisha yak kwamba, mfumo wa kidijitali unaozidi kuboreshwa na NMB ni kati ya mabadiliko ya aina yake kuwahi kufanywa na taasisi za kifedha nchini na kwamba BoT haitosita kuisapoti NMB katika kufikia malengo yak kidijitali iliyojiwekea.
“BoT tunaahidi ushirikiano kwa NMB katika sio tu kufikia malengo yao, bali pia katika kuhakikisha inapunguza idadi ya Watanzania wasiotumia huduma za kibenki. Mandeleo kuelekea Uchumi wa Kati, yanahitaji ushiriki wa kila Mtanzania,” alisema Dk Kibesse.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, alisema uzinduzi wa huduma hizo ni nafasi nyingine yak NMB kuboresha huduma zake matawini na nje ya matawi na kwamba wamejipanga kuwafikia Watanzania popote walipo.
Aliongeza kwamba wanajivunia mabadiliko yak kimfumo yanayofanya upatikanaji wa huduma uwe mikononi mwa Watanzania popote walipo na kwamba anaamini NMB Klik App, NMB Scan Pay na ufunguaji akaunti kwa simu za mkononi, utachagiza maendeleo yao.
Alisisitiza kuwa, katika kuhakikisha wanabaki kuwa kinara wa huduma za kibenki nchini, watahakikisha wanapokea na kuufanyia kazi ushauri wowote watakaopata kutoka kwa wateja, ambao watabaki kuwa kipaumbele chao katika kuanzisha huduma mpya.
Ili kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi, mteja atapaswa kutembelea menu ya NMB Mobile, ambako atafuata maelekezo na kwa watumiaji wa simu za Android na Iphone watapakua App ya NMB Klik kupitia Google Play Store na App Store.
No comments:
Post a Comment