Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiwaongoza viongozi wengine
kutembelea eneo la mwambao wa Ziwa Victoria
baada ya kuikabidhi boti hiyo ya doria kwa Jeshi la Polisi, kutoka
kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Geita, Daniel Shilla, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na Diwani wa Chato, Richard Bagolele. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Geita, Daniel Shilla akimshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni baada ya kumkabidhi Kituo cha Polisi kinachohamishika wilayani
Chato.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyeshika koti), akishuka katika boti maalumu
aliyowakabidhi Kikosi cha Polisi wilayani Chato ikiwa ni mkakati wa Serikali
kupambana na uhalifu katika ukanda wa Ziwa na Bahari nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi
Robert Gabriel, akishuka katika boti maalumu iliyokabidhiwa na Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) kwa Kikosi
cha Polisi Wanamaji wilayani Chato,
ikiwa ni mkakati wa Serikali kupambana na uhalifu katika ukanda wa Ziwa na
Bahari nchini.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment