Mkuu wa Mkoa Ally Hapi akisalimia na wazee wa Wilaya ya Kilolo
alipofanya ziara yake ya kujitambulisha wilayani humo.
MKuu
wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah akisoma taarifa Wilaya kabla ya
kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Ally Hapi, alipofanya ziara wilayani hapo kwa
ajili ya kujitambulisha. (Picha zote na
Datus Mahendeka).
NA Datus Mahendeka (OuT)
MKUU mpya wa Mkoa wa
Iringa, Ally Hapi, amesema atahakiki na ufanisi wa utendaji wa kila mtumishi au
mkuu wa Idara ndani ya Wilaya ya Kilolo.
Akizungumza na
watumishi na wakuu wa Idara mbalimbali wa Wilaya ya Kilolo katika ziara yake ya
kwanza ya utambulisho ambapo alisema, lengo kubwa ni kuijenga Iringa mpya.
“Kwangu kila mtu
atabeba mzigo wake mwenyewe, na ile dhana na kupeana taarifa kwa makaratasi
tutaona uhalisia wake pindi tukija site (eneo la mradi),
ili taarifa hizo ziwe sambamba na kinachonekana”alisema
Alifafanua kuwa,
amepanga ratiba ya siku 18 zenye lengo la kutembelea kila Tarafa, kukagua,
kufungua, kufuatilia miradi ya maendeleo ndani ya Wilaya zote za Iringa.
Alisema Mkurugenzi ni
vyema kuwa na taarifa za kila wiki za watendaji wake ikiwemo wamefanya nini au
wiki ijayo wanatarajia kufanya kitu gani ili mishahara na posho walipwe kwa
haki.
Alisema ni vyema
watendaji hao waaachana na utendaji wa mazoea, kutengeneza chuki baina ya
Serikali na Wananchi kutokana na kutoshughulikia matatizo ya watu.
Aliongeza kuwa uzoefu
unaonyesha kuna baadhi ya watendaji hawajatatua mgogoro wa aina yoyote ndani ya
sehemu yake, hivyo ni lazima wawe mfano kwa kuatua na kuwa ripoti ya wiki ya
utendaji wao wa kazi.
Aidha, alisema ni
vyema watendaji hao na wakuu wa vitengo kwenda kwa Wananchi badala ya kukaa ofisi,
ili kujiridhisha na taarifa zenye kusifia kuwa hali ni nzuri.
Aliongeza kuwa wakuu
wa Idara wana vitendea kazi mbalimbali ikiwemo magari, hivyo ni lazima
wazunguke kwa Wananchi kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua kero zao.
Pia aliwataka kuwa
waadilifu, kutojihusisha na vitendo vya rushwa kutoka kwa Wananchi kwani wanalipwa
mshahara kutoka kwa Wananchi hao, pamoja na kutunza siri mbalimbali za ofisi na
taarifa za vikao.
Aliongeza kuwa
ushirikiano baina ya watendaji na wakuu wa Idara na watumishi wengine itakuwa
nguzo ya maendeleo na kutimiza lengo la kuwa Iringa mpya.
Hata hivyo
aliwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya kwenye Nyanja mbalimbali za maendeleo
ikiwemo elimu na kilimo.
No comments:
Post a Comment