HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 13, 2018

CRDB BANK YAMWAGA SERA KWA WAJASIRIAMALI WANAWAKE WAFUGA KUKU-MKURANGA MKOANI PWANI

Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala jijini Dar es Salaam, Midlaster Nsanzugwanko, akizungumza na Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga wakati wa ufunguzi wa semina yao, ya siku mbili, iliyoandaliwa na Jukwaa la Wanawake Mkuranga na kufunguliwa na Mbunge wao, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, ukumbi wa Flex Gardern, wilayani humo jana. Kulia ni Kaimu Meneja Biashara, Adrian Kongojole na kushoto ni Afisa Mauzo wa tawi hilo, Mohammed Madengelo. CRDB Bank imedhamini semina hiyo. 
Baadhi ya Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, wakimsikiliza Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala, Midlaster Nsanzugwanko, alipokuwa akizungumza nao kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo, kwa wateja wake, wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Afisa Mauzo wa CRDB Bank, tawi la Mbagala, Mohammed Madengelo, akielezea sera za benki hiyo, kwa Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, wakati wa ufunguzi wa semina yao, ya siku mbili inayoendelea ukumbi wa Flex Gardern.
Wajasiriamali wanawake wafuga kuku kutoka sehemu mbalimbali za Wilaya ya Mkuranga, wakimsikiliza Afisa Mauzo wa CRDB Bank, tawi la Mbagala, Mohammed Madengelo. 
Kaimu Meneja Biashara wa CRDB Bank, Adrian Kongojole, akigawa vipeperushi vya benki hiyo, kwa washiriki wa semina ya Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa wilaya ya Mkuranga.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya uuzaji wa vyakula na dawa za mifugo ya Farmers Centre, Salim Msellem, akizungumza na wanasemina, Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, alipokuwa akitoa sera ya kampuni yake. Kampuni hiyo, ni moja wa wadhamini wa semina hiyo.
Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala, Midlaster Nsanzugwanko (kushoto) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga, Mariam Ulega, wakifurahia jambo wakati akimuonesha kitu katika kipeperushi cha benki hiyo, wakati wa semina hiyo. 
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina ya siku mbili ya Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akimtambulisha Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala, Midlaster Nsanzugwanko (kushoto) kwa Mkuu wa wilaya hiyo, Filberto Sanga (wa pili kulia), walipofika ukumbi wa Flex Gardern kwa ufunguzi wa semina hiyo. 
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akizungumza wakati akiifungua semina hiyo, ya Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa wilayani Mkuranga jana. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Mhandisi Msham Munde, akiwa na mkewe, Amina Munde, wakiionesha zawadi aliyokabidhiwa na Jukwaa la Wanawake, Mkuranga, kutokana na juhudi zake za kusaidia kusonga mbele jukwaa hilo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jikwaa, Christina Mrema.  
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akimkabidhi cheti maalum cha Mwanamke Bora, wilayani Mkuranga, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga, Mariam Ulega, mara baada ya kuifungua rasmi semina hiyo. 

No comments:

Post a Comment

Pages