Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimpongeza Mwanariadha wa Polisi
Fabian Nelson baada ya kumpandisha cheo kutoka Kostebo mpaka Koplo kutokana na
kufanya vizuri katika Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika
Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na
wanariadha Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki
(EAPCCO) iliyomalizika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla
ya kuwapongeza Wanamichezo wote kwa kuchukua nafasi ya pili kwa ujumla.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipokea kombe la ushindi wa pili kwa
ujumla kutoka kwa Inspekta Hashim Abdallah lililopatikana katika Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda
wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es
Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza Wanamichezo wote kwa kuchukua nafasi ya
pili kwa ujumla.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipokea kombe la ushindi wa kulenga
Shabaha kutoka kwa mwakilishi wa Walenga shabaha walioliwakilisha Jeshi la
Polisi Tanzania katika Michezo ya Wakuu
wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika mwishoni
mwa wiki Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza Wanamichezo wote
kwa kuchukua nafasi ya pili kwa ujumla. (Picha na Jeshi la Polisi).
Na Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini IGP Simon Sirro amempandisha Cheo Mwanariadha wa Polisi Fabian Nelson
kutoka Konstebo hadi Koplo baada ya kuchukua medali ya dhahabu na kuvunja rekodi ya mbio za mita 5000 katika
Michezo ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki
(EAPCCO) iliyomalizika mwishoni mwa wiki
Jijini Dar es Salaam.
Mwanariadha huyo
alikimbia dakika 13: 45: 99 na kuwashinda Wanariadha wa Jeshi la Polisi la
Kenya na Uganda ambapo Tanzania ilishika
nafasi ya pili katika ushindi wa jumla ambapo nafasi ya kwanza ilienda Kenya
na ya tatu Uganda.
IGP Sirro alimpandisha
Cheo hicho katika hafla ya kuwapongeza Wanamichezo walioshiriki Michezo hiyo
katika bwalo la Maafisa wa Polisi Oystabya IGP Sirro alisema mwanariadha huyo
amekuwa akionyesha juhudi katika mbio ndefu jambo ambalo limekuwa likileta sifa
kwa Jeshi la Polisi na nchi kwa Ujumla.
“ KIla mmoja anastahili pongezi kutokana na
kutuwakilisha vizuri katika michezo hii, hivyo tunathamini mchango wa kila
mmoja kwa nafasi yake katika kuitangaza nchi yetu na nawaahidi tutaendelea
kutambua mchango wa kila mmoja” Alisema Sirro
Aidha, Alisema
maandalizi ya michezo ijayo yanaanza sasa ili kuhakikisha kuwa wanaendelea
kufanya vizuri zaidi na kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika
michezo ya mwaka huu ikiwemo kuingia kambini mapema na kuajiri wanamichezo
pindi nafasi zitakapopatikana.
Kwa upande wake Kamishna
wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa alisema kazi iliyofanyika ni kubwa na kila
mshiriki alijituma kuhakikisha kuwa Vikombe na medali zinabaki hapa nchini.
Michezo inayoshindaniwa
ni pamoja na soka ,mpira wa mikono, mpira wa wavu, mpira wa pete, Ngumi,
Taekwondo, Judo na Riadha ambapo nchi zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Sudani, Sudani Kusini na Tanzania.
No comments:
Post a Comment