·
Mechi zote 380 kwenye ‘live’ HD ndani ya Bomba
·
Pia Mechi zote 380 za La Liga kuonekana
·
Mechi 108 za Ligi ya Uingereza (EPL) nzao ndani ya Kifurushi cha Bomba
Siku
chache tu kabla ya kuanza kwa moja ya ligi maarufu Duniani – Ligi kuu
ya Italia Serie A, MultiChoice imetangaza neema ya burudani kwa wateja
wake kwa kuweka michezo yote 380 ya
ligi hiyo katika kifurushi cha chini kabisa cha DStv Bomba ambacho
hulipiwa shilling 19,000 tu kwa mwezi.
Kama
hiyo haitoshi, DStv pia itaonyesha mechi zote 380 za ligi ya Hispania –
La Liga katika kifurushi hicho cha bomba huku mechi 108 za ligi kuu ya
uingereza (EPL) nazo zikionyeshwa
katika kifurushi hicho cha chini kabisa.
“Kama
ilivyo ada, sisi DStv kila uchao tunahakikisha kuwa tunamfikishia
mtanzania burudani popote alipo na kwa gharama nafuu. Hii ndiyo sababu
tumeamua kuiweka ligi hii maarufu katika
kifurushi chetu cha Bomba kinachopatikana kwa shilingi 19,000 tu kwa
mwezi” amekaririwa Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria.
“Tunatambua
kuwa ligi ya Italia ni moja ya ligi zenye mvuto mkubwa ulimwenguni na
kama kawaida kwa kupitia DStv, tunawafanya watanzania kuwa sehemu ya
ulimwengu wa burudani hususan soka,
hivyo tumeamua kwa makusudi kabisa kuiweka ligi hii ya italia kwenye
kifurushi cha bomba” amebainisha Alpha.
Wiki
iliyopita DStv ilitangaza kuirejesha ligi hiyo ya Italia na kuweka
michezo michache kwenye kifurushi cha Bomba, lakini kutokana na maoni ya
wateja wake wengi, imeamua kuishusha
ligi hiyo katika kifurushi cha chini kabisa.
Ligi
Kuu ya Italia inatarajiwa kuanza Jumamosi hii ambapo washabiki wa soka
watamshuhudia mwanasoka nguli Christiano Ronaldo akiiwakilisha timu
maarufu ya Juventus kwa mara ya kwanza.
Mtanange huo wa ufunguzi utakuwa kati ya Juventus na Chievo na
utaonyeshwa mubashara kupitia DStv chanel ya SuperSport 8 (HD)
Mbali
na hayo, wateja wa DStv wataendelea kufurahia msimu huu mpya wa soka
na katika kunogesha zaidi michuano ya ligi ya uingereza itatangazwa kwa
lugha ya kiswahili.
Ili
kuwapa wateja wake uhuru zaidi wa kufurahia soka popote walipo, DStv
inaendelea kutoa huduma ya DStv Now ambapo mteja wa DStv anaweza
kutazama
matangazo katika vifaa zaidi ya vinne kama vile simu, kompyuta, na
televisheni ya kawaida.
No comments:
Post a Comment