.Shughuli za kiuchumi zaongezeka
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Timbolo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha DC, Samwel
Kivuyo, akifafanua jambo wakati kwa waandishi wa habari waliotembelea
kijiji hicho kuangalia miundombinu ya mawasiliano iliyowekwa na Kampuni
ya Halotel. Kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Josephine Mhina.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda (katikati),
akiwaelekeza wakazi wa Kijiji cha Timbolo namna ya kutumia huduma za
mtandao wa Halotel wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutembelea
miundombinu ya kampuni hiyo.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Wakazi wa kijiji cha Timbolo,Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha,
wamepongeza jitihada za mtandao wa simu wa Halotel kwa kufikisha mawasiliano kijijini
hapo baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kupata huduma za Mawasiliano ya uhakika
jambo ambalo limechangia kwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa
kijiji hicho hususani huduma jumuishi za fedha(financial inclusion).
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa
kijiji hicho, Bw. Samwel Kivuyo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali walipokwenda kutembelea katika kijiji hicho ili
kuona na kujifunza shughuli mbalimbali za kimaendeleo ambazo zimechangiwa na
mtandao huo kuwekeza katika maeneo ambayo awali hayakuwa na huduma za
mawasiliano ya uhakika.
‘’Halotel wamesaidia sana kufikisha
huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi masikini wa kijiji hiki ambao awali
walikuwa wanataabika na kupitwa na huduma hizo hivyo kulazimika kutembea
kilometa nyingi kufuata huduma za kifedha,kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji
hicho, Bw. Samwel Kivuyo.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji hicho
katika kata ya Sambasha,wameelezea kufurahishwa na huduma ya Halopesa,ambapo
wamesema,imekuwa rafiki kulinganisha na huduma kama hizo zinazotolewa na kampuni
nyingine,kufutia Halotel kutotoza makato pindi mtumiaji wa huduma hiyo akituma
pesa kwenda mtandao huo.
“ Kwakweli ukiwa na huduma za Haloteli,unafurahia
kupata muda wa maongezi wa kutosha,data ndiyo siwezi kuelezea,yaani ni huduma
rafiki sana kwa sisi hasa wa huku kijijini ambao kipato chetu ni cha chini. Alisema,Rehema
Joshua,mkazi kijiji cha Timbolo,kata ya Sambasha,Wilaya ya Arumeru,mkoa wa
Arusha.
"Sisi kama wananchi wa Timbolo
tunashukuru kwanza kabisa jitihada za serikali kwa kuiwezesha kampuni ya Halotel kuweza kuweka minara ya mawasiliano katika
kijiji chetu ili wananchi waweze kupata huduma za mawasiliano katika maeneo yao
na kusaidia wananchi kutumia huduma za mawasiliano katika kujiendeleza kiuchumi
kwani hapo awali hatukuwa na huduma ya mawasiliano ya uhakika.,"
Mpaka sasa hali ya mawasiliano katika
kijiji chetu ni nzuri, watu wamepata ajira kufuatia kuanzisha biashara za
huduma za kifedha kwa njia ya simu pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao
ya mboga mboga ambayo ni kazi kuu ya wanakijiji wetu, kwani mara ya kwanza
mawasiliano na wafanyabiashara wengine yalikuwa ni magumu ila sasa tuna uhakika
wa wateja kwa sababu tunawasiliana nao moja kwa moja na hata upokeaji wa malipo
umekuwa ni rahisi. Alisema Kivuyo na kuongeza.
"Tunafurahi sana kuwa na mradi
wa mawasiliano katika kijijj chetu kwa sababu miundo mbinu ya mawasiliano
iliyojengwa na Halotel .Katika kijiji chetu imesaidia wananchi kuimarisha
usalama katika maeneo mbalimbali ya kijiji chetu kwani imekuwa rahisi kupeana
taarifa mbalimbali katika kijiji chetu. Alisema
Aidha Mwenyekiti huyo alibainisha
kuwa hadi sasa changamoto inayowakabili kijijini hapo ni Ukosefu wa umeme
katika kijii hicho jambo ambalo linatatiza shughuli za maendeleo kwa baadhi ya
wananchi.
“Tunaomba Wakala wa umeme
vijijini(REA) watusaidie kupata umeme hasa katika kitongoji cha Meduti na
Murerian ili wananchi waweze kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo na
kijamii,ikiwemo kilimo, uchomeleaji wa
vyuma, shuleni, vituo vya afya ili
wananchi waweze kuboresha maisha yao na kujiongezea kipato katika kijiji
hicho kilichoanzishwa mwaka 1972 chenye
wakazi 4638 na jumla ya kivitongoji vinne ambavyo ni Oltingidi,
Madukani, Meduti na Muterian”,alisema mwenyekiti huyo.
Baada ya kuzungumza na mwenyekiti
huyo wa kijiji cha Timbolo,kuhusiana na kadhia hiyo ya umeme,waandishi walimtafuta mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry
Muro,kutaka kufahamu namna serikali inavyoweza
kuwasadia wananchi hao,ambao tayari wameshafanya jitihada za kufungiwa mfumo wa
umeme majumbani mwao.
“Kwakweli nawapongeza wananchi hao wa
kijiji cha Timbolo,kwa jitihada zao na serikali inafurahishwa mno na ana ya
wanachi wanaopenda kujiletea wenyewe maendeleo,na nimemtaka mwenyekiti wa kijji
cha Timbolo, Samwel Kivuyo,aje wakati wowote ofisni kwangu akiwa na wawakilishi
watatu wa wanakijiji waje tuzungumze na kumaliza mara moja kadhia hiyo ya umeme”,alisema,mkuu
wa Wiayaya Arumeru, Jerry Muro.
Wakati huo huo mkuu wa Idara ya
Mawasilianno,Kampuni ya Halotel Tanzania, Mhina Simwenda alisema kuwa kampuni
ya Halotel Tanzania ipo mkoani Arusha kwa ajili ya kuongea na wateja,kusikiliza
maoni kutoka kwao, kujua wanahitaji nini, kujua changamoto walizonazo
ili waweze kuboresha huduma zao kwa wateja.
"Ukiangalia kijiji cha Timbolo
ndiyo chenye mafanikio mazuri katika suala la mawasiliano na sisi kama Halotel
Tanzania tunaishukuru serikali ya kijiji cha Timbolo kwa kuunga mkono juhudi za
kampuni yetu ili tuweze kuleta huduma za mawasiliano hapa kijijini," alisema,
Semwenda.
No comments:
Post a Comment