Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndugu Philip
Mangula akiwa na Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) Mhe. John
Momose Cheyo wakiwa ndani ya ndege ya Rais kabla ya kuondoka kuelekea
mjini Harare, Zimbabwe, kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa
nchi hiyo Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa zinazofanyika leo Jumapili
Agosti 26, 2018.
Katika safari hiyo viongozi hao wanafuatana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) ambaye atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
k2:
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipanda ndege
ya Rais tayari kuelekea mjini Harare, Zimbabwe, kumuwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulikwenye kwenye
sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo Mhe. Emmerson
Dambudzo Mnangagwa zinazofanyika leo Jumapili Agosti 26, 2018. PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment