Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (katikati), akisalimiana na baadhi ya
wafanyakazi wakati alipowasili katika ofisi za wilaya ya Karagwe kabla ya
kutembelea jana pori la akiba Kimisi katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua
ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika pori hilo lililopandishwa
hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa,
Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Godfrey Luheluka.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga, akisaini kitabu cha wageni mara
alipowasili katika ofisi za wilaya ya Karagwe kabla ya kutembelea jana
pori la akiba Kimisi katika ziara yake
ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya
kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika pori hilo lililopandishwa hadhi
kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja
na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngala pamoja na baadhji
ya watumishi wa TAWA na TANAPA wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana pori hilo katika ziara
yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa
ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika hilo.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa ramani inayoonesha Ziwa Ngozi
ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika Pori la Akiba la Kimisi na
aliyekuwa Meneja wa Pori hilo Bigilamungu Kagoma wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana pori hilo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua
ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika
pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa.
NA LUSUNGU
HELELA-KAGERA
Baada ya kuyapandisha
hadhi mapori matano ya akiba, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet
Hasunga amewataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa
ya kuwekeza katika Mapori hayo.
Aidha, Amesema
Serikali imefuta kodi ya kuingiza magari ya watalii nchini ili
kuwawezesha wananchi walio wengi kuingia katika biashara hiyo ikiwa lengo ni
kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya Utalii.
Ametaja aina ya
uwekezaji unaohitajika kuwa ni ujenzi wa hoteli zenye hadhi ya nyota moja hadi
zenye nyota tano, nyumba za kulala wageni, uanzishwaji wa makampuni ya utalii
pamoja na kutoa huduma za vyakula kwa ajili ya watalii.
Ametoa rai hiyo leo
wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Karagwe mkoani
Kagera kabla ya kutembelea ziwa Ngoma ambalo ni miongoni mwa vivutio vya
utalii vilivyopo katika Pori la Akiba la Kimisi ambalo ni miongoni mwa mapori
yaliyo katika mchakato wa kuwa hifadhi za taifa.
Naibu waziri huyo
anatembelea mapori ya mkoa wa Kagera kufuatilia hatua iliyofikiwa na Hifadhi za
Taifa Tanzania (TANAPA) katika kuyaendeleza.
Amesema Mapori ya
Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika ni hazina na fursa kwa
mikoa ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania kufunguka kiutalii kwa wananchi wa
maeneo hayo na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment