Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) jana akimsikiliza
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.
Richard Mayongela (watatu kushoto) alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na
Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani
Simiyu.
Mshauri wa Sera za Miundombinu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bi. Pudencia (kushoto) jana akimsikiliza kwa
makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
Bw. Richard Mayongela akimweleza masuala mbalimbali alipotembelea banda la
Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye
Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Kamati ya maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane ya Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), jana alipotembelea banda la Mamlaka katika
Uwanja wa Nyakabindi. Kulia waliokaa ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw.
Richard Mayongela.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Jumanne
Sagini (wa pili kushoto) akipata taarifa ya ujenzi wa Kiwanja kipya cha Ndege
cha mkoa huo kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Bw. Alex Kalumbete jana alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na
Sherehe za Nanenane yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),(mwenye suti nyeusi) jana
alipotembelea banda lao la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane
yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment