Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw.
Paul Rwegasha akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela katika michezo ya bonanza la uzinduzi wa mazoezi
ya michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI), lililofanyika leo
kwenye viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi),
Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho (aliyesimama) akizungumza na wanamichezo wa
Sekta ya Uchukuzi walioshiriki leo kwenye bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya michezo
Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) lililofanyika katika viwanja vya
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza Johari (wa pili
kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi Dkt Leonard
Chamuriho (wa tatu kushoto) akiwa katika bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya michezo
ya Wizara, Idara na Taasisis za Serikali (SHIMIWI), lililofanyika leo kwenye
viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Wa pili kushoto ni
Mwenyekiti mpya wa Klabu ya Uchukuzi, Bw. Alphonce Mwingira.
Timu ya wanawake ya kuvuta Kamba ya Uchukuzi wakivutana na wenzao ambao hawapo
pichani katika bonanza la uzinduzi wa michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali
(SHIMIWI), lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA).
Timu
ya wanaume ya kuvuta Kamba ya Uchukuzi wakivutana na wenzao ambao hawapo
pichani katika bonanza la uzinduzi wa michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali
(SHIMIWI) lililofanyika leo kwenye Viwanja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza Johari
(mbele namba 11) akiwafanyisha mazoezi watumishi kutoka taasisi mbalimbali
zilizopo chini ya Sekta ya Uchukuzi, katika bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya
Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI), yaliyofanyika leo kwenye
viwanja vya TCAA. Wa kwanza kulia mbele
ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho.
No comments:
Post a Comment