Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia), akisaini mkataba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Nguyen Van Son, utakaowezesha shule zaidi ya 200 za serikali kupata kompyuta na inteneti bure, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko Halotel, Mhina Semwenda na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd. (Picha na Francis Dande).
NA MWANDISHI WETU
BENKI
ya NMB kwa kushirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, zimeingia mkataba
wa miaka miwili utakaowezesha shule zaidi ya 200 za Serikali kupata kompyuta na
mtandao (network) bure, kwa lengo la kuboresha mfumo wa kujifunza na
kufundishia kupitia teknolojia.
Mkataba
huo ulisainiwa jana jijini Dar es Salaam, ambako Mkurugenzi Mtendaji wa NMB,
Ineke Bussemaker, alisema benki yake itatoa kompyuta 350 kwa shule 100 kwa sasa,
ambazo kwa kandarasi hiyo, maana yake zitaunganishwa na mtandao wa Halotel.
“Hii
ni huduma endelevu, ambapo kwa miaka minne iliyopita NMB ilitoa msaada wa
kompyuta zaidi ya 600 mashuleni na changamoto ikawa mtandao. Sasa kwa mkataba
huu, maana yake Halotel itakuwa na jukumu la kupita na kuunganisha mtandao,”
alisema Ineke.
Aliongeza
kuwa benki yake itatoa jumla ya kompyuta 400 kwa mwaka huu, ambazo kwa
kujumlisha na hizo zilizotolewa awali, Halotel wataziunganisha na mtandao ili
kuwaweza waallimu na wanafunzi kufundisha na kujifunza kwa ufanisi.
“Kwa
miaka mingi sasa NMB kupitia Kitengo cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), imejikita
katika kusaidia sekta kadhaa ikiwemo ya elimu kwa kuchangia madawati, vitabu,
kompyuta, ujenzi wa vyumba vya kujisomea na kwa ushirikiano huu, tunaamini
tutaenda mbali zaidi,” alisema.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi ya Halotel, Nguyen Van Son, alisema
wanafurahishwa na ushirikiano wao na NMB katika kufanikisha upatikanaji wa
mtandao mashuleni na kwamba hiyo sio mara ya kwanza kwa wao kuunga mkono
jitihada za kunyanyua elimu nchini.
Aliongeza
kwamba, wanaamini ushirikiano wao na NMB utakuwa chachu ya walimu kupenda
kufundisha na wanafuzi kupenda kujifunza, hivyo kuchagiza kiwango cha ufaulu na
kunyanyua elimu ya Tanzania kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(Tehama).
No comments:
Post a Comment