NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya BASF kwa kushirikiana na Taasisi ya
Kimataifa ya Kuboresha Lishe (GAIN), wameandaa warsha itakayowakutanisha pamoja
wadau ili kujadiliana namna ya kupunguza kasi ya sumu kuvu nchini Tanzania.
Miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa katika warsha
hiyo ni pamoja na Hatari kubwa ya usalama wa chakula na usalama katika nchi
zinazoendelea ni sumu kuvu, ambako warsha itachunguza ufumbuzi wa kusambaa kwa
kasi kwa sumu kuvu nchini Tanzania
Enock Musinguzi, ambaye Mwakilishi Mkazi wa GAIN, alisema
jijini Dar es Salaam jana kuwa warsha hiyo inalenga kuendeleza mkakati wa
kitaifa wa kupambana na sumu kuvu, ambapo itawajumuisha pia wadau kutoka nchi
nyingine.
Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja
wa Mataifa (FAO), sumu kuvu ni hatari kubwa kwa usalama wa chakula na usalama
katika nchi zinazoendelea.
Sumu kuvu maarufu kama Aflatoxin, ni aina ya sumu
inayotengenezwa na ukungu katika nafaka iliyohifadhiwa katika sehemu ambayo
kitaalamu haijakidhi vigezo vya kuhifadhia, sumu ambayo huwa na athari kwa
wanadamu, wanyama na husababisha ugonjwa wa ini na saratani.
Musinguzi alibainisha ya kuwa kukosekana kwa mavuno,
usafiri na utunzaji sahihi, ni miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa kasi kwa
sumu kuvu, ambako ulimwenguni, inakadiriwa kati ya watu bilioni 4 hadi 5 wapo
hatarini kuathiriwa na sumu kuvu.
“Watoto ni miongoni mwa waathirika wakubwa, kwani
sumu kuvu huwa inasababisha upunguvu wa virutubisho, udumavu na maendeleo ya
ukuaji wa mtoto. Kupitia warsha hii, wadau watajifunza masuala mbalimbali
kuhusiana na changamoto hii,” alisema Musinguzi.
Naye Dk. Andreas Bluethner, ambaye ni Mkurugenzi wa
Chakula, Usanifu na Ubia wa BASF, alisema moja ya malengo ya warsha hiyo ni kusaka
ufumbuzi wa thamani ya chakula ili kuendeleza upunguzaji wa chakula na kuongeza
usalama na chakula cha lishe kufikia SDG2.
"Kama kujitolea kwetu kwa Malengo ya Maendeleo
ya Umoja wa Mataifa (SDG), tunaendelea kufanya kazi na wadau muhimu kwa
ufumbuzi wa thamani ya chakula ili kuendeleza ufumbuzi wa kupunguza chakula na
kuongeza usalama na chakula cha lishe kufikia SDG2 ya njaa ya sifuri.
“Kwa mtazamo huu, BASF na washirika wake wameunda
udongo wa sumu kuvu ambao unaweza kuongezwa kwa vyakula vidogo vidogo na
inaweza kupunguza upungufu wa sumu hiyo,” alisisitiza Bluethner.
No comments:
Post a Comment