HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 26, 2018

NSSF Yashiriki Maonyesho ya Kwanza ya Madini mkoani Geita

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limeshiriki maonyesho ya kwanza ya madini yanayoendelea mkoani Geita kwa lengo la kuwafikia kwa ukaribu zaidi watanzania wote watakaoshiriki maonyesho hayo kwaajili ya kutoa elimu na kuandikisha.

Maonyesho haya ambayo yameshirikisha wadau wote wa sekta ya madini yameanza tarehe 24 hadi tarehe 30 mwezi Agosti katika viwanja vya kalangalala mkoani Geita.

Kufuatia mabadiliko ya sheria NSSF sasa inalenga kuandisha wale wote waliopo sekta binafsi ya ajira na sekta isiyo rasmi, ili wanufaike na mafao yatolewayo na shirika hili ikiwemo fao la matibabu bure kwa mwanachama na familia yake.

Akiongea kutoka viwanja vya kalangalala meneja wa NSSF Mkoa wa Geita Bwana Shaban Mpendu ametoa wito kwa watanzania wote kutembelea maonyesho hayo ya migodi na kufika katika banda la NSSF ili kuweza kupata elimu ya mafao yanayotolewa na NSSF pamoja na elimu ya hifadhi ya jamii kwa ujumla. Vilevile meneja amewataka wananchi hasa wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi kujiandikisha na NSSF. Uandikishaji unaofanyika katika banda la NSSF ni pamoja na uandikishaji wa waajiri, wanachama na usaijili wa matibabu bure.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita, Shaban Mpendu,  akimpa maelezo mafupi mgeni rasmi Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini alipotembelea banda la NSSF katika Maonyesho ya Madini mkoani Geita. 



No comments:

Post a Comment

Pages