Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB, Patrick Msusa, akizungumza katika mahafali ya 18 ya TIOB.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB, Patrick Msusa, akitoa hotuba yake katika mahafali hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, ambaye alikuwa mgeni rasmi akitoa hotuba yake.
Picha ya pamoja.
Wahitimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB, Patrick Msusa, akitoa hotuba yake katika mahafali hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker ambaye alikuwa mgeni rasmi akitoa hotuba yake.
Baadhi ya wahitimu.
Wahitimu.
Wahitimu.
Wahitimu.
Wahitimu.
Wajumbe wakiwa katika mkutano wa Mwaka wa TIOB ulioenda sambamba na mahafali ya 18 ya Taasisi ya Taaluma ya Kibenki Tanzania (TIOB).
Mhitimu wa Taasisi ya Taaluma ya Kibenki Tanzania (TIOB), Emmanuel Mwakafwila, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo TIOB, Martina Revelian, wakati wa mahafali ya 18 yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wahitimu wa Mafunzo ya Ngazi ya Juu ya Kibenki, Givens Ernest, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo wa TIOB, Martina Revelian, wakati wa mahafali ya 18 ya Taasisi ya Taaluma ya Kibenki Tanzania (TIOB) yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wahitimu wa Mafunzo ya Ngazi ya Juu ya Kibenki, Givens Ernest, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo wa Taasisi ya Taaluma ya Kibenki Tanzania (TIOB), Martina Revelian, wakati wa mahafali ya 18 yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wahitimu wa Mafunzo ya Ngazi za Juu ya Kibenki kutoka Taasisi ya Taaluma ya Kibenki Tanzania (TIOB), Chibby Chibby, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo TIOB, Martina Revelian, wakati wa mahafali ya 18 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, jumla ya wahitimu 157 walitunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali.
Wahitimu wakiwa na furaha.
NA MWANDISHI WETU
WAHITIMU wa Taasisi ya Taaluma ya Kibenki Tanzania (TIOB) wametakiwa kuzingatia weledi na kutoa huduma bora kwa wananchi na wawekezaji.
Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, katika mahafali ya 18 ya TIOB, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema utoaji huduma bora, wenye lengo moja la kuhakikisha Watanzania na wawekezaji wanapata mafanikio na kukuza uchumi wa nchi.
Ineke aliwataka wahitimu hao kuzingatia weledi na kusimamia walichofundishwa ili kuboresha sekta hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB, Patrick Msusa, alisema wanafunzi 157 wamehitimu masomo ya kibenki katika ngazi mbalimbali.
ngazi ya juu ya taaluma ya kibenki na wawili wametunukiwa vyeti vya kubobea katika masomo maalum ya kibenki,”alisema.
Alisema wahitimu wengi ni wafanyakazi katika taasisi za fedha nchini na wengine ni wale wanaojiandaa kuingia katika soko la ajira.
“TIOB imekuwa ikitoa mafunzo ya elimu ya kibenki kwa wafanyakazi pamoja na wanafunzi kwa lengo la kuwaongezea ufanisi na uwezo katika utendaji wao wa kazi,”alisema Mususa.
Alisema, sifa ya kujiunga na masomo katika ngazi ya cheti ni lazima uwe na elimu kuanzia shahada ya kwanza ya benki na kwa ngazi ya ubobezi ni kwa ajili ya kuwaandaa wafanyakazi hasa wale wanaotarajia kupandishwa cheo, kwani masomo hayo yanawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.
Mususa alisema changamoto iliyopo kwa baadhi ya wamiliki wa mabenki nchini ni kuajiri watu wanaohitimu vyuo bila kupitia TIOB ili wapikwe kimaadili.
“Tunawashauri wenye mabenki wanapoajiri wafanyakazi wapya wawalete TIOB,”alisema Mususa.
TIOB ilianzishwa mwaka 1993 kwa sheria ya makampuni (Companies Ordinance - Cap 212) baada ya kuonekana umuhimu wa kuwa na chombo cha kitaifa cha kusimamia taaluma ya kibenki hasa baada ya kufungua milango kwa taasisi za fedha za kimataifa kuwekeza Tanzania.
No comments:
Post a Comment