Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjukuu
wa Malkia wa Uingereza Prince William mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar
es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
mazungumzo na mgeni wake Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William
aliyeambatana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke pamoja na ujumbe
wake mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni
Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na Waziri wa
Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjukuu wa
Malkia wa Uingereza Prince William mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mjukuu wa
Malkia wa Uingereza Prince William picha ya wanyama wanaopatikana katika mbuga
mbalimbali nchini mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mjukuu wa Malkia
wa Uingereza Prince William Kamusi ya Kiswahili mara baada ya kuwasili Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya
Picha kutoka kwa Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William Ikulu jijini Dar
es Salaam. Picha hiyo inamuonesha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere akiwa anazungumza na Malkia wa Uingereza Elizabeth II -PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment