Na
Mwandishi Wetu
KLABU
ya michezo ya Uchukuzi (USC) imeanza kujifua kwa ajili ya kushiriki mashindano
ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Wakala
wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), itakayoanza Septemba 25
kwenye viwanja mbalimbali mkoani Dodoma.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Bw. Mbura Tenga amesema wameanza kujifua
kwa nguvu ili kurudi na ubingwa wa michezo mbalimbali waliyoshinda kwa mara ya
mwisho michezo hiyo ilipofanyika mwaka 2014.
Bw.
Tenga amesema USC watashiriki kwenye michezo tisa, ambayo imeandaliwa na
SHIMIWI, ambayo ni mpira wa miguu, netiboli, kuvuta Kamba, riadha, bao, karata,
draft, baiskeli na Darts.
“Tunauhakika
wa kwenda kufanya vizuri kwani timu imeanza mazoezi tayari ingawa muda ni
mdogo, ila ninaamini tutafanya vizuri,” amesema Bw. Tenga.
USC
inatetea vikombe vinne walivyoshinda mwaka 2014, ambavyo ni Darts –
wanaume(washindi wa kwanza); mpira wa miguu (washindi wa pili); na Kamba –
wanaume na baiskeli - wanawake (washindi wa tatu).
Ratiba
iliyotolewa na SHIMIWI inaonesha katika ufunguzi mabingwa watetezi katika
mchezo wa kuvuta Kamba wanaume timu ya Ofisi ya Rais Ikulu itavutana na MSD;
nao wanawake wa RAS Iringa ambao ni mabingwa watetezi watavutana na Viwanda;
huku katika mpira wa miguu Wizara ya Elimu watakutana na Ukaguzi.
Michezo
hiyo ambayo pamoja na kuunganisha wafanyakazi wa umma wa maeneo mbalimbali pia
huleta burudani kwa wakazi wa eneo husika.
Katibu
wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Vallery Chamulungu (wa
kwanza kulia) akiwa ni miongoni mwa wachezaji wa klabu ya Uchukuzi walioanza
mazoezi jana nyuma ya jengo la Aviation wakijiandaa na mashindano ya Shirikisho
la Michezo ya Wizara, Idara za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI),
iliyopangwa kufanyika mkoani Dodoma kuanzia Septemba 25, 2018.
Bi. Sharifa Amiri (kulia) akifanya mazoezi
ya mchezo wa bao na Bw. Ambakise Mwasunga jana kwenye viwanja vya nyuma ya Jengo la Aviation wakijianda
na mashindano ya Shirikisho la michezo ya Wizara, Idara za Serikali na Ofisi za
Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), iliyopangwa kuanza Septemba 25, 2018 mkoani Dodoma.
Wachezaji wa timu ya wanawake na wanaume ya
kuvuta Kamba ya Klabu ya Uchukuzi (USC) wakifanya mazoezi jana nyuma ya jengo
la Aviation Banana ya kujiandaa na mashindano ya Shirikisho la Michezo ya
Wizara, Idara za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), iliyopangwa
kuanza Septemba 25 mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment