Kwa
niaba ya Shirikisho la Riadha Tanzania napenda kumpa pongezi za dhati
bosi wangu Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Anthony Mtaka (pichani), kwa kazi nzuri
anayoifanya katika kutimiza wajibu wake alioaminiwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.
Familia
ya Riadha imepata faraja kubwa pale ambapo kazi za kiongozi wao mkuu
inampa Rais furaha hadi kumtaja hadharani kwamba ni Mkuu wa Mkoa bora
Tanzania.
Juhudi
za Mtaka hazijaishia Mkoani Simiyu pekee; Mtaka ni kiongozi wa kitaifa
wa Shirikisho muhumu la michezo nchini, Shirikisho pekee ambalo
limeiletea taifa sifa kubwa kwa kupeperusha bendera ya Tanzania
kimataifa.
Pia
Mtaka ameiletea heshima kubwa Tanzania kwa kuhamasisha Diplomasia ya
Kimichezo (Sports Diplomacy) kimataifa. Matokeo ya kazi nzuri anazofanya
sasa Tanzania imepewa uenyeji wa Mashindano ya Africa ya Mbio za Nyika
(2020 Africa Cross Country Championships).
Mimi
Mtendaji wake Mkuu kwa upande wa RT nafahamu kabisa uwezo wake katika
kila jambo analokusudia, ataamka usiku wa manane, atapiga simu kushauri
hadi lengo litimie.
Natoa
wito kwa vijana wenzangu ambao wameaminiwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, wawatumikie wananchi na kubuni mbinu mpya za
maendeleo ya maeneo yao, hiyo ndiyo itakuwa zawadi nzuri mbele ya Mungu
na mbele ya Rais.
Nawasihi
viongozi chipukizi waepuke kuiga mambo ya kuonyesha hasira zao ili
waonekane kwenye mitandao, haisaidii kabisa, yanaudhi sana maana wengine
hata mwezi hawajatimiza tangu wateuliwe lakini ninahofu watatumbuliwa
muda wowote. "Mtaka siyo Mtata" Mtaka anachapa kazi.
Wilhelm Gidabuday,
Katibu Mkuu - RT.
Katibu Mkuu - RT.
No comments:
Post a Comment