NA TIGANYA VINCENT
JUMLA ya wanawake 46,158 mkoani Tabora wamejifungua katika kipindi cha kuanzia Januari hadi kufikia Septemba mwaka huu.
Kauli
hiyo imetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu wa Afya wa Mkoa wa Tabora
Tausi Yunge wakati wa mkutano wa wadau wa faya wa Mkoa huo.
Alisema
walijifungua chini ya umri wa miaka 20 walikuwa 11,332 ambao ni sawa na
asilimia 24.5 na wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya ishirini
waliojifungua walikuwa 34,826 sawa na asilimia 75.4.
Tausi
alisema watoto waliozaliwa wakiwa hai walikuwa 45,336 sawa na asilimia
98.7 na wasio hai walikuwa 563 sawa na asilimia 1.2.
Kaimu
Katibu Afya Mkoa huyo alisema jumla ya wanawake waliojifungulia katika
vituo vya kutolea huduma walikuwa ni 43,991 sawa na asilimia 95.3.
Wakati
huo huo Kaimu Katibu huyo wa Afya Mkoa amesema kuwa hadi hivi sasa ni
Wazee 32,470 sawa na asilima 50 ya wazee 71,116 ya waliotambuliwa ndio
wameshapewa vitambulisho kwa ajili ya matibabu mkoani humo.
Alisema
ni Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ndio inaoongoza kwa kutoa kwa wazee
6,700 kati ya 9,766, kufuatiwa na Kaliua iliyotoa kwa wazee 3,700 kati
ya 6,019, Uyui 4,000 kati ya 6,840 na Urambo imetoa kwa wazee 5,120
kati ya 9,387.
Tausi
alisema Halmashauri ambazo bado ziko chini ni Manispaa ya Tabora ambayo
imetoa vitambulisho kwa wazee 600 kati 9,475, Sikonge imetoa kwa wazee
600 kati ya 3,580, Mji Nzega imetoa kwa wazee 1,803 kati ya 5,421 na
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imetoa kwa 9,947 kati 20,628.
Kufuatia
zoezi hilo kwenda polepole Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa
wiki moja kwa wahusika wote kuhakikisha wamekamilisha kazi ya utoaji wa
vitambulisho kwa wazee wote wanaonzia miaka sitini na kuendelea.
Alisema baada ya muda huo kupitia ataanza kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika nafasi zao wanaohusika.
No comments:
Post a Comment